Shirika lisilo la kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI imeungana na serikali ya mkoa wa Shinyanga kuadhimisha Siku ya UKIMWI duniani Desemba 1,2019 kwa kutoa huduma mbalimbali zinazolenga kupunguza maambukizi mapya ya VVU.

 
Maadhimisho hayo kwa mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack. 
 
AGPAHI imeshiriki katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kwa kutoa elimu ya VVU na UKIMWI na maonesho ya shughuli zinazofanywa na AGPAHI ikiwemo ujasiriamali kwa vijana wanaolelewa na shirika hilo. 

 

Wauguzi na wakunga kutoka vituo vya afya,hospitali na zahanati mkoa wa Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya uanzishaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (Nurse Initiated Management of Anti – Retroviral Therapy – NIMART) ili waweze kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na UKIMWI. 

 
Mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku 10 yameanza leo Jumanne Novemba 19,2019 katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja wauguzi 28 kutoka halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC). 
 
Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI. 
 
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mark Ogweyo amesema yanalenga kuwajengea uwezo wauguzi na wakunga nchini ili waweze kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na UKIMWI,ikiwemo kuwaanzia dawa za kufubaza makali ya VVU. 
 
“Kupitia mafunzo hayo wauguzi na wakunga watasaidia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha nchi kufikia malengo ya 90-90-90 ya VVU na UKIMWI ifikapo mwaka 2020 ambapo lengo ni kuhakikisha watu wanapima VVU, kutumia dawa na kufubaza makali ya VVU”,alisema Ogweyo. 
 
“Tunataka ifikapo mwaka 2020, asilimia 90% ya watu wenye maambukizi ya VVU wamefikiwa na kupimwa,ambapo asilimia 90% ya walioapata maambukizi watapewa dawa za kufubaza virusi (antiretroviral treatment) na asilimia 90% ya watakaotumia dawa hizo hawataweza kuwaambukiza wenza watakaojamiiana nao kwa sababu virusi vitakuwa vimefubazwa na tiba hiyo”,alieleza Ogweyo. 

Page 1 of 40

More on News

Get Connected