Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) imeendesha kikao kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za mradi wa DREAMS unaolenga kuwafikia mabinti wa rika balehe na wanawake wadogo katika vituo 12 vya kwenye halmashauri za wilaya za Ushetu,Msalala,Kahama Mji na Manispaa ya Shinyanga. 

Kikao hicho cha siku mbili kimefanyika Februari 21 na 22,2019 katika ukumbi wa Virgimark Hotel Mjini Shinyanga kwa kukutanisha pamoja mabinti wenye umri kati ya miaka 15 – 19pamoja, wanawake wadogo wenye umri wa miaka 20 -24 na watoa huduma kwenye vituo vya afya.

 
Watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga wametakiwa kuongeza juhudi za kuwatafuta,kuwarudisha na kuhakikisha Watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI waliopotea katika huduma wanaendelea kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU.
 
Wito huo umetolewa Februari 19,2019 na Mratibu wa Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha wakati akifunga warsha ya Watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga.
 
Warsha hiyo iliyodumu kwa muda wa siku tatu iliyoandaliwa na Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) ilijikita zaidi katika kujadili na kupanga mikakati namna ya kukabiliana na changamoto ya wateja kupotea katika huduma. 

Mwezeshaji wa Huduma za VVU na UKIMWI katika jamii kutoka Manispaa ya Shinyanga, Mwita Thomas.
 
Viongozi wa dini wameombwa kuacha kupotosha jamii kuhusu Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI kuwa mtu anayeishi na VVU akiombewa virusi vinapotea mwilini. 
 
Ombi hilo limetolewa leo na watoa Huduma za VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga, wakiwa kwenye warsha ya kuwajengea uwezo ili kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC) iliyoandaliwa na Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI). 
 
Walisema baadhi ya Viongozi wa dini wamekuwa wakiwadanganya watu wanaoishi na maambukizi ya VVU waache kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) kwa madai kuwa maombi yanawaponya. 

More on News

Get Connected