Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Magoma ambaye ndie alikua mgeni rasmi katika hafla ya kufunga kambi ARIEL CAMP 2018, akiingia huku akiwa ameambatana na watoto, vijana, wafanyakazi wa AGPAHI pamoja na wauguzi waliokua wakiwaangalia watoto na vijana wakati wakiwa kambini.

Jumatatu ya Tarehe 12/13/2017 Shirika lisilo la Kiserikali la Arial Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)   lilianza kambi maalumu ya watoto na vijana wa Mikoa mitatu ya Tanzania kati ya Mikoa sita inayofanya kazi na shirika la AGPAHI. Leo, tarehe 16/03/2018 ikiwa imetimia siku ya tano tokea mafunzo hayo ya kambi ya watoto yaanze.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Best Richard Magoma alifunga mafunzo hayo ya watoto na vijana katika hafla fupi ya ufungaji wa kambi hiyo inayojulikana kama ARIEL CAMP 2018 huku ikiwa na kauli mbiu “KIJANA EPUKA TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU.”

 

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akiwa katika picha ya Pamoja na Vijana na Watoto Nje ya Ukumbi wa hotel ya Uhuru iliyopo Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Toka mwaka 2011 Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekua msaada mkubwa kwa watoto wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini Tanzania. Shirika hili la kitaifa lisilo la Kiserikali lilianzishwa na shirika la Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation  (EGPAF) huku lengo kuu likiwa kutokomeza maambukizo ya virusi vya Ukimwi kwa watoto nchini Tanzania. Mpaka sasa AGPAHI ina takribani miaka saba, shirika hili limekua msaada mkubwa kwa watoto hao wanaoishi na VVU kutimiza ndoto zao. 

 

Mratibu wa kudhibiti UKIMWI mkoa wa Simiyu Dr. Khamis KulembaAkifungua Warsha ya siku tatu kwa Waviu washauri (Watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi washauri) iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi. 

Baadhi ya Waviu Washauri (Watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi washauri) kutoka katika Wilaya tano za Mkoa wa Simiyu wakiendelea na mafunzo yanayotolewa na Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi. 

Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi limeendesha warsha ya siku tatu kwa Waviu Washauri (Watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi washauri) kutoka wilaya za Busega na Maswa Mkoa wa Simiyu.
Warsha hiyo ilishirikisha jumla ya Waviu washauri 24 kutoka katika wilaya za Busega,Maswa, ambapo lengo likiwa ni kuwaongezea ujuzi na mbinu za kuwashawishi watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi waliocha kutumia dawa kuendelea na matumizi ya dawa.

More on News

Get Connected