Watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu wameweka kambi ya siku tano mkoani Kilimanjaro ili kupatiwa maarifa mbalimbali yatakayowawezesha kukua na kuishi katika matumaini chanya,Mwandishi wetu Kadama Malunde,anaripoti Zaidi. 

Kambi hiyo inayoitwa Kambi ya Ariel ni ya sita kufanyika tangu shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu na Geita lilipoanzishwa mwaka 2011.
Kambi hiyo imeanza siku ya Jumatatu,Juni 13,2016 katika hoteli ya Lutheran Uhuru mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo maafisa kutoka AGPAHI ,madaktari bingwa wa watoto,wataalaamu wa masuala ya kisaikolojia,wasimamizi wa watoto kutoka vituo vya afya na baadhi ya waandishi wa habari walihudhuria.


Hapa ni katika uwanja wa taifa Mjini Kahama mkoa wa Shinyanga ambapo Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative(AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI limefanya Bonanza la Michezo kwa vijana.Bonanza hilo limewakutanisha vijana 120 kutoka Vituo vya Afya vilivyopo katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji


Bonanza hilo lililofanyika Jumamosi,Mei 21,2016 liliandaliwa na AGPAHI likiwezeshwa na Mfuko wa Kusaidia watoto wa Uingereza ( Children’s Investment Fund Foundation UK- (CIFF) limekutanisha vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19,ambao wapo katika rika balehe,rika ambalo ni muhimu sana katika jamii.

Mgeni rasmi katika Bonanza hilo la Michezo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa.Wengine waliohudhuria Bonanza hilo ni waganga wakuu wa halmashauri za wilaya ya KahamaMji,Ushetu na Msalala,wasimamizi wa klabu za vijana,vijana,wafanyakazi wa AGPAHI na wakazi wa Kahama.

Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu limekutana na wafamasia na waratibu wa shughuli za maabara katika halmashauri za wilaya za mikoa hiyo katika kikao cha sita cha robo cha mwaka.

Kikao hicho cha siku mbili kimefanyika katika ukumbi wa Karena Hotel uliopo mjini Shinyanga,ambapo tarehe 05 Mei,2016 shirika hilo limekutana na wafamasia na wataalam wa maabara kutoka mkoa wa Simiyu na Mei 06,2016 likakutana na wafamasia na wataalam wa maabara kutoka mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho Mratibu wa Madawa na Mifumo ya Ugavi kutoka AGPAHI, Emilian Ng’wandu (pichani hapo juu) alisema lengo la kikao hicho cha sita cha kazi ni kupata taarifa kutoka katika halmashauri hizo kuhusu shughuli za usambazaji dawa na vifaa tiba katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma, kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili mafanikio na njia za kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa kutekeleza shughuli mbalimbali zihusuzo mfumo wa ugavi katika wilaya husika.

More on News

Get Connected