Serikali mkoani Mwanza imeitaka jamii kote nchini kuwapeleka watoto wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) shule, badala ya kuwanyanyapaa na baadhi kuwaficha ndani na kisha kufifisha ndoto zao za maisha.

 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Leonard Subi, akifungua kambi Siku tano Jiji Mwanza, kushoto kwake Mkurugeni wa (AGPAHI) Dkt. Sekela Mwakyusa.

Akizungumza katika kambi ya siku tano mjini hapa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt Leonard Subi kwenye ufunguzi wa kambi hiyo iliyotayarishwa  na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya ‘Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) na kuwakutanisha watoto 50 wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka mikoa ya Tanga, Simiyu na Mara, Dkt. Subi amehimiza umuhimu wa malezi kwa watoto

“Naamini kila mtoto ana ndoto zake  katika maisha lakini zaidi sana katika kusoma na vipaji vingine endapo tu akisaidiwa kwa kujengewa mazingira rafiki ya kumwezesha kupata elimu bila bugudha, alisema Dkt..Subi na kuongeza “Kila mtoto ana haki ya kuishi, apate afya bora”.

Picha ya pamoja katika maadhimisho ya kifua kikuu -  Mererani.

 

Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojishughulisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeungana na wadau wote duniani katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani, 24 March 2017.

Maadhimisho hayo yalifanyika katika mji mdogo wa Mererani, wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara, eneo ambalo Shirika la AGPAHI linatekeleza mradi wa kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI sehemu za migodini kwa hisani ya shirika la ADPP la Msumbiji.

Katika maadhimisho hayo, shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na timu ya afya ya wilaya walifanya zoezi la kutoa huduma mbalimbali kwa jamiii inayozonguka mji mdogo wa Marerani kuanzia tarehe 23 – 25 Machi, 2017.

Huduma zilizotolewa ni uchunguzi wa kifua kikuu, kupima Virusi vya Ukimwi na kutoa elimu kwa umma kuhusu kifua kikuu na VVU/UKIMWI.

Zoezi hilo lilisimamiwa na afisa mradi wa kifua kikuu na UKIMWI, kutoka AGPAHI, mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Simanjiro, wataalamu wa maabara, watoa huduma wa Afya kutoka kituo cha Afya Mererani na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

Maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani “World TB Day” mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika machimbo ya dhahabu ya Nyangarata kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama.
 
Maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yamefanyika Machi 24,2017 katika kitongoji cha Nyangarata,kijiji cha Kalole kata ya Lunguya ambapo kuna shughuli za uchimbaji wa madini.
 
Maadhimisho hayo yameandaliwa na timu ya afya mkoa wa Shinyanga na za wilaya kwa ushirikiano mkubwa wa shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Geita,Mara,Mwanza na Tanga.
 
AGPAHI pia ni wadau wa muda mrefu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu nchini Tanzania.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya ‘Tuungane Kutokomeza Kifua Kikuu’ alikuwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

More on News

Get Connected