Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano kwa ajili ya matibabu ya akina mama wanaogundulika na dalili za awali za maambukizi ya kansa ya shingo ya kizazi (Cryotherapy Machine) katika halmashauri za Sengerema, Kwimba na Ilemela mkoani Mwanza.Huduma hii hutolewa katika vituo vya kutolea huduma ya afya 20 katika mkoa wa Mwanza

Pia shirika hilo limekabidhi kompyuta 18 kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kutunzia taarifa za matumizi ya dawa za kufubaza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ARV’s pamoja na magonjwa nyemelezi.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa hii leo kwenye mkutano wa wadau wanaosaidia mapambano ya Ukimwi mkoani Mwanza, uliofanyika Jijini Mwanza ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI Dr. Sekela Mwakyusa anafafanua zaidi kuhusiana na vifaa hivyo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Magoma ambaye ndie alikua mgeni rasmi katika hafla ya kufunga kambi ARIEL CAMP 2018, akiingia huku akiwa ameambatana na watoto, vijana, wafanyakazi wa AGPAHI pamoja na wauguzi waliokua wakiwaangalia watoto na vijana wakati wakiwa kambini.

Jumatatu ya Tarehe 12/13/2017 Shirika lisilo la Kiserikali la Arial Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)   lilianza kambi maalumu ya watoto na vijana wa Mikoa mitatu ya Tanzania kati ya Mikoa sita inayofanya kazi na shirika la AGPAHI. Leo, tarehe 16/03/2018 ikiwa imetimia siku ya tano tokea mafunzo hayo ya kambi ya watoto yaanze.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Best Richard Magoma alifunga mafunzo hayo ya watoto na vijana katika hafla fupi ya ufungaji wa kambi hiyo inayojulikana kama ARIEL CAMP 2018 huku ikiwa na kauli mbiu “KIJANA EPUKA TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU.”

 

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akiwa katika picha ya Pamoja na Vijana na Watoto Nje ya Ukumbi wa hotel ya Uhuru iliyopo Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Toka mwaka 2011 Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekua msaada mkubwa kwa watoto wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini Tanzania. Shirika hili la kitaifa lisilo la Kiserikali lilianzishwa na shirika la Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation  (EGPAF) huku lengo kuu likiwa kutokomeza maambukizo ya virusi vya Ukimwi kwa watoto nchini Tanzania. Mpaka sasa AGPAHI ina takribani miaka saba, shirika hili limekua msaada mkubwa kwa watoto hao wanaoishi na VVU kutimiza ndoto zao. 

More on News

Get Connected