Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’ mkoa wa Mwanza.
 
 

Msaada huo umetolewa Jumanne Machi 27,2018 katika ukumbi wa mikutano wa Gold Crest Hotel jijini Mwanza wakati wa kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kupanga mipango na mikakati ya kupambana na VVU na Ukimwi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema mashine hizo ni kwa ajili ya vituo vya afya vya Katunguru na Kabila vilivyopo wilaya ya Sengerema, hospitali ya Ngudu iliyopo wilayani Kwimba na zahanati ya Kirumba na kituo cha afya cha Buzuruga vilivyopo wilayani Ilemela.
 
Dk. Sekela alisema mashine hizo tano zenye thamani ya shilingi milioni 6.8 zitatumika kutolea tiba mgando kwa akina mama wanaokutwa na dalili za mwanzo za kansa ya uzazi.
 “Mbali na shirika letu kuendelea kuboresha huduma za kinga na matunzo pia tunatoa huduma ya uchunguzi wa dalili saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama”,alieleza.
 
Alisema huduma hiyo hutolewa katika vituo vya kutolea huduma ya afya 20 katika mkoa wa Mwanza.
Dk. Sekela alisema shirika hilo mpaka sasa limetoa msaada wa ‘cryotherapy machines’ 17 katika mikoa sita ambayo ni Mwanza,Shinyanga,Tanga,Geita,Simiyu na Mara zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 115.6.
 
Dk. Sekela pia alikabidhi kompyuta 18 zitakazotumika kuhifadhi takwimu za wateja wa CTC katika vituo vya afya husika na kusaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka na kwa usahihi Zaidi mkoani Mwanza.
 “Tangu tuanze mradi wa Boresha, tutakuwa tumetoa jumla ya kompyuta 82 kwa mkoa wa Mwanza ambazo zinatumika kutunza taarifa za watu wenye VVU na Ukimwi”,alisema.

 

Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano kwa ajili ya matibabu ya akina mama wanaogundulika na dalili za awali za maambukizi ya kansa ya shingo ya kizazi (Cryotherapy Machine) katika halmashauri za Sengerema, Kwimba na Ilemela mkoani Mwanza.Huduma hii hutolewa katika vituo vya kutolea huduma ya afya 20 katika mkoa wa Mwanza

Pia shirika hilo limekabidhi kompyuta 18 kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kutunzia taarifa za matumizi ya dawa za kufubaza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ARV’s pamoja na magonjwa nyemelezi.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa hii leo kwenye mkutano wa wadau wanaosaidia mapambano ya Ukimwi mkoani Mwanza, uliofanyika Jijini Mwanza ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI Dr. Sekela Mwakyusa anafafanua zaidi kuhusiana na vifaa hivyo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Magoma ambaye ndie alikua mgeni rasmi katika hafla ya kufunga kambi ARIEL CAMP 2018, akiingia huku akiwa ameambatana na watoto, vijana, wafanyakazi wa AGPAHI pamoja na wauguzi waliokua wakiwaangalia watoto na vijana wakati wakiwa kambini.

Jumatatu ya Tarehe 12/13/2017 Shirika lisilo la Kiserikali la Arial Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)   lilianza kambi maalumu ya watoto na vijana wa Mikoa mitatu ya Tanzania kati ya Mikoa sita inayofanya kazi na shirika la AGPAHI. Leo, tarehe 16/03/2018 ikiwa imetimia siku ya tano tokea mafunzo hayo ya kambi ya watoto yaanze.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Best Richard Magoma alifunga mafunzo hayo ya watoto na vijana katika hafla fupi ya ufungaji wa kambi hiyo inayojulikana kama ARIEL CAMP 2018 huku ikiwa na kauli mbiu “KIJANA EPUKA TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU.”

More on News

Get Connected