Wanawake wakiwa katika banda la Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya VVU/ Ukimwi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo kitaifa yalifanyikia mkoani Simiyu. 

Utafiti wa mwaka jana, uliofanywa na kituo cha habari cha saratani ya mlango wa  kizazi Tanzania (HPV Information Centre), unabainisha kuwa wanawake 9,772 wengi wao wakiwa na umri wa kuanzia miaka 40-64 waligundulika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi hapa nchini.

Kila mwaka inakadiriwa kuwa wanawake 6,695 wengi wao wakiwa na umri wa miaka 15-44 wanapoteza maisha kutokana na saratani hiyo ikiwa ni asilimia 22.4 ya waathirika wote nchini.

Wataalumu wa masuala ya afya wanasema saratani ya mlango wa  kizazi hutokea katika chembechembe za shingo ya kizazi, ambayo ni sehemu ya chini ya mji wa mimba (uterus).

Takwimu za Kituo cha Kudhibiti Maradhi Duniani (CDC), za mwaka 2008 zinaonesha kuwa katika kila wanawake watatu, wawili kati yao wanashambuliwa na saratani ya aina hii duniani. Hapa nchini, inakadiriwa kuwa zaidi ya wanawake milioni 14 walio katika umri wa kuzaa kuanzia miaka 18 hadi 25 wapo hatarini kupata saratani ya shingo ya kizazi.

More on News

Get Connected