Vijana wanaotoka katika halmashauri za wilaya ya Kahama Mji,Ushetu,Msalala na Manispaa ya Shinyanga wamekutana katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

Bonanza hilo la michezo limejumuisha vijana 150 wenye umri kati ya miaka 14-19 wanaotoka katika klabu za vijana zilizoundwa na zinasimamiwa na shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya husika.

Akifungua bonanza hilo katika uwanja wa taifa mjini Kahama leo Jumamosi Desemba 17,2016,mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama,alisema bonanza hilo ni kwa ajili ya vijana kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha vipaji na kujifunza.

Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative( AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limefanya mkutano na wabunge wanaotoka mikoa ya Shinyanga , Simiyu na Geita kwa lengo la kuwafahamisha watunga sera kazi zinazofanywa shirika hilo katika mikoa hiyo ikiwa ni pamoja na kuainisha mafaniko yaliofikiwa katika kipindi cha miaka mitano (5)tangu lilipoanza kutekeleza miradi yake mwaka 2011. 

Mkutano huo umefanyika siku ya Jumanne, Agosti 23, 2016 mjini Dodoma ukiwa ni wa tatu kufanyika tangu kuanzishwa kwa shirika la AGPAHI mwaka 2011, likifadhiliwa na watu wa Marekani kupitia mashirika ya Centres for Disease Control and Preventation (CDC); shirika la misaada la Marekani (USAID); Mfuko wa kusaidia watoto wenye VVU kwa hisani ya watu wa Uingereza (CIFF) na Mfuko wa Idadi ya watu duniani (UNFPA).

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni wawakilishi wa kamati ya Bunge inayoshuhulika na masuala ya Ukimwi (TAPAC) na wabunge waliohudhuria mkutano huo ni Mhe. Stanslaus Nyongo, Mhe. Esther Midimu, Mhe. Ezekiel Maige, Mhe. Augustino Masele, Mhe. Elias Kwandikwa, Mhe. Dunstan Kitandula na Mhe. Shally Raymond.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa aliwaeleza waheshimiwa wabunge kuwa miongoni mwa kazi zinazofanywa na AGPAHI kuwa ni pamoja na kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) hususani kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kutoa huduma ya matunzo na tiba kwa watu wanaoishi na VVU katika mikoa ya Shinyanga , Simiyu na Geita.


Kambi ya Ariel ya mwaka 2016 (Ariel Camp 2016) iliyodumu kwa muda wa siku tano kwa watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu iliyoandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi imefungwa.

Kambi hiyo ya 6 iliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Watoto na Vijana ni hazina : Wape Kipaumbele katika huduma za afya na makuzi ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU", ilianza siku ya Jumatatu,Juni 13,2016 na kumalizika siku ya Ijumaa, Juni 17,2016.

 Lengo la kambi ilikuwa kuwapatia watoto na vijana maarifa mbalimbali yatakayowawezesha kukua na kuishi katika matumaini chanya.

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo katika viwanja vya Hoteli ya Lutheran Uhuru mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa ambaye pia ni rais wa Chama Cha Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania, alisema washiriki wa kambi hiyo ni watoto na vijana kutoka klabu 50 za watoto kutoka kwenye kliniki za huduma za dawa na matunzo katika mikoa hiyo.

More on News

Get Connected