Shirika la AGPAHI lilifanya ziara ya kutembelea Bohari ya dawa (MSD) kanda ya ziwa, ikiwa ni sehemu ya warsha ya siku tatu kwa WAVIU washauri wanaotoka katika mkoa wa Shinyanga. Lengo la ziara hii lilikuwa kuwawezesha WAVIU washauri kufahamu kazi za ununuzi, utunzaji na usambazaji wa dawa zinazofanywa na MSD.

Katika ziara hiyo, WAVIU waliuliza maswali mbalimbali ikiwemo kutaka kujua ukweli kuhusu uhalali wa dawa zilizokwisha muda wake na kama zina muda wa ziada wa miezi mitatu hadi sita kuweza kutumika (Bw. Kanzaga Fabian kutoka kituo cha CTC ya Segese) 

Watu wanaoishi wa virusi vya UKIMWI (WAVIU) wanaoendelea kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi wameaswa kuwafuatilia wenzao ambao wameacha kutumia dawa hizo ili warejee na kuendelea kutumia huduma.

Akizungumza kwenye warsha ya kuwajengea uwezo watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga, mkurugenzi wa miradi wa shirika la AGPAHI, Dkt. Amos Nsheha amesema kuacha kutumia dawa hizo ni kuhatarisha maisha yao.

More on News

Get Connected