Kaimu Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI mkoa wa Shinyanga Sherida Madanka akizungumza wakati wa kufunga warsha ya siku tatu kwa WAVIU Washauri kutoka halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga.

Jumla ya WAVIU Washauri 75 kutoka halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga wamepatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma na kuwarudisha kwenye huduma za tiba na matunzo.

Mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa serikali ya Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control and Preventation (CDC) yalianza Januari 29,2018 na kumalizika Januari 31,2018 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kufunga warsha hiyo na kugawa vyeti vya ushiriki, Kaimu Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Shinyanga Sherida Madanka, aliwataka WAVIU Washauri kujitambua na kutoa elimu kuhusu haki za WAVIU katika jamii. Aidha aliwaasa WAVIU Washauri kutunza siri za wateja wanaowahudumia na kuhakikisha wanakuwa viongozi wa kuigwa katika jamii. 

“Ninaamini mtakwenda kutumia elimu mliyopata kuiemilisha jamii, mnatakiwa muwe kioo cha jamii ili wananchi wapate pa kukimbilia, hakikisheni mnatunza siri za watu mnaowahudumia”,alisisitiza Madanka. 

Alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la AGPAHI kwa huduma linalozotoa katika kutekeleza miradi ya Ukimwi huku akibainisha kuwa shirika hilo limekuwa kimbilio la wengi na mdau mkubwa wa masuala ya afya kwa serikali ya Tanzania. 

Shirika lisilo la kiserikali Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limemaliza warsha ya siku tatu kwa WAVIU Washauri 46 kutoka kwenye halmashauri nne za mkoa wa Geita.

WAVIU washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa, kutoa ushauri nasaha kwa wenzao, kujitolea kufuatilia na kufundisha wenzao kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha WAVIU wenzao kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.

Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita,Dk Joseph Odero akizungumza na WAVIU washauri wakati wa warsha ambapo aliwasisitiza kutumia vyema mafunzo hayo

 

Akizungumza katika warsha hiyo, Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Mkoani Geita, Dr Joseph Odero aliwasisitiza WAVIU Washauri kutumia uchache wao kuleta chachu kwenye jamii ambazo wamekuwa wakishughulika kufanya kazi za ushauri kwa watu ambao wanaishi na maambukizi ya VVU.

“Mwaka 2017 kwa mkoa wa Geita asilimia kumi na nne (14%) ya watu walikua wanaishi na maambukizi ya VVU na themanini na mbili (82%) walikuwa ni wazima sasa tumeona kumbe kwa kutumia dawa mambo yanawezekana. Lakini pia tumeona wengine wameendelea kwenda kwa waganga wa jadi hawataki kukubali kwamba wanaishi na VVU hali hii nyie kama WAVIU washauri mnajukumu la kuhakikisha manawasaidia watu wenye hali hiyo”, alisema Dr. Odero.

Odero ameendelea kusisitiza uzoefu ambao wameupata kwa siku tatu kutumia vyema mafunzo hayo na yaonekane kuleta tija kwenye jamii ambazo wanatokea kwani kufanya hivyo watakuwa wamewasaidia watu ambao wanaishi na maambukizi ya VVU kujiona kuwa wanathamani kwenye jamii.

 

Serikali imewaagiza watumishi  wa sekta ya Afya katika mkoa wa Shinyanga na Geita,kutumia  vizuri fedha za miradi ya ukimwi zinazotolewa na wafadhili ili ziweze kuwafikia walengwa na kuacha tabia ya kujinufaisha wenyewe kupitia fedha hizo.

 Wito huo umetolewa leo na mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr Rashid Mfaume kwa niaba ya makatibu tawala wa mkoa wa Shinyanga na Geita,wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya usimamizi wa fedha yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI.

 Dr Mfaume amesema kumekuwa na tabia ya badhi ya watumishi wa Afya kutumia fedha za miradi ya wafadhili kwa kujinufaisha wenyewe huku walengwa wakikosa huduma muhimu ambazo zimekusudiwa kuwafikia.

 Sambamba na hayo Dr Mfaume amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa wa Shinyanga na Geita kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya ukimwi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watumishi watakaotumia vibaya fedha hizo.

More on News

Get Connected