SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la AGPAHI linalojihusisha na maswala ya UKIMWI katika mikoa wa Shinyanga, Simiyu na Geita limewataka watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI mkoani Simiyu kuacha kujinyanyapaa wenyewe na badala yake wajitokeze kuchukua dawa kwa uwazi pasipo kificho. 

Wito huo umetolewa jana (10/03/2015) jijini Mwanza na Kaimu Mkurugenzi wa AGPAHI, Dr. Sarah Matemu katika warsha ya WAVIU washauri iliyoandaliwa na Shirika hilo kwa lengo la kuwapa mbinu mpya za kuwashauri na kuwarudisha kwenye huduma watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Gari Jipya, aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop yenye nambari za usajili DFPA 912 limetolewa na Shirika la AGPAHI kwa msaada wa watu wa marekani kwa ajili ya kusaidia shughuli za UKIMWI katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.

 


Meneja wa miradi wa AGPAHI wa mikoa ya Simiyu na Shinyanga, Dr. Gastor Njau akitoa maneno machache ya utangulizi. Walio meza kuu, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa AGPAHI, Bwana Laurean Bwanakunu, Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Georgina Bundala na Mkurugenzi wa Wilaya Dr. Leonard Masale.

More on News

Get Connected