Kambi ya Watoto na Vijana “Ariel Camp” iliyoandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi iliyoanza June 19,2017 jijini Mwanza imefungwa leo Ijumaa June 23,2017.

Kambi hiyo ilikutanisha watoto na vijana 50,walezi 11 walioambana nao kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita. Miongoni mwa mambo waliyojifunza katika kambi hiyo iliyodumu kwa muda wa siku tano ni pamoja na lishe,ufuasi mzuri wa dawa,unyanyapaa na ubaguzi,haki na wajibu wa watoto pamoja na elimu ya afya ya ujana na makuzi. Washiriki wa kambi hiyo pia walitembelea makumbusho ya Wasukuma ya Bujora na kufanya michezo mbalimbali nje ya darasa yenye kuashiria umoja,ushirikiano,upendo na kujenga mtazamo chanya kwenye maisha yao.

Akizungumza wakati wa kufunga kambi ya nane ya Ariel jijini Mwanza,mgeni rasmi,Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura, aliwataka watoto na vijana hao kuwa mabalozi wazuri wanaporudi nyumbani huku akiwasihi kuzingatia masomo na kanuni za afya ili kufikia malengo yao ya kimaisha.

Katika hatua nyingine,Dk. Wambura alisema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na shirika la AGPAHI katika sekta ya afya na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao ili watanzania wengi zaidi waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na shirika hususani katika mapambano ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.

 

 
Watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Geita,Mwanza na Shinyanga wanaoshiriki katika kambi ya Ariel 'Ariel Camp 2017’ jijini Mwanza iliyoandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi, wametembelea makumbusho ya kabila la Kisukuma ‘Sukuma Museum’ ya Bujora Kisesa Mwanza ili kujifunza tamaduni na mila za Kisukuma.

Mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) Dk. Safila Telatela akizungumza wakati wa kufungua Ariel Camp (Kambi ya Ariel) ya siku tano kuanzia June 19,2017 - June 23,2017 iliyokutanisha watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita jijini Mwanza.

 

         Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Mwanza Dk. Pius Maselle akifungua kambi ya watoto na vijana 'Ariel Camp' katika hotel ya Lesa Garden jijini Mwanza.Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Gastor Njau akifuatiwa na Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita Dk. Joseph Odero. Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Mwanza, Olympia Laswai akifuatiwa na Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela. 

                                                                                          *****

More on News

Get Connected