Serikali mkoani Shinyanga imepongeza kazi zinazofanywa na shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI katika juhudi zake za kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bwana Ally Rufunga wakati alipotembelewa na Rais na mtendaji mkuu wa EGPAF,Bwana Chip Lyons ofisini kwake mjini Shinyanga.

Rufunga amesema kuwa shirika la AGPAHI limefanya mambo mengi katika mapambano dhidi ya maambukizi ya ukimwi mkoani humo ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vya matunzo na matibabu (CTC) Kwa watu wanaoishi na VVU.

Sambamba na hayo Rufunga amesema kuwa Serikali peke yake haiwezi kupambana na kasi ya maambukizi ya ukimwi na kuongeza kuwa uwepo wa Shirika la AGPAHI umesaidia kupunguza kasi ya maambukizi kwa mkoa wa Shinyanga.

More on News

Get Connected