WAZAZI NCHINI WATAKIWA KUACHA KUWAFICHA WATOTO WANAOHITAJI HUDUMA ZA AFYA.

 

Mgeni rasmi wa tukio la ufunguzi wa kambi, Mganga Mkuu wA Mkoa wa Mwanza Dkt. Lenard Subi wakiwa katika picha ya pamoja

Wazazi na walezi wametakiwa kutowaficha watoto wanaohitaji huduma za afya kwakuwa huduma hizo zinatolewa bure na serikali katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za umma, hayo yamesemwa leo,Tarehe 15 na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Dkt. Leonard Subi katika ufunguzi wa kambi ya watoto inayoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Initiative (AGPAHI).

Dkt. Subi amesema, huduma za watoto zinatolewa bure lakini wapo baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwaficha watoto kwa kutokuwapeleka katika vituo vya afya hali inayopelekea kusababisha ongezeko la vifo vya watoto nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa, amesema shirika hilo limekuwa likishiriki kutoa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ambapo wameweza kuwafikia watu 189,806 kati yao watoto wakiwa 8615, ambayo ni sawa na asilimia 5%.

Dkt. SEKELA MWAKYUSA amesema kambi hiyo ambayo ni ya saba kuandaliwa na shirika la AGPAHI, itadumu kwa muda wa siku tano, jijini Mwanza. Kambi hiyo iliyoanza jumatatu, 15 Mei 2017, imewakutanisha watoto 50 kutoka mikoa ya Tanga, Simiyu na Mara ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa watoto juu ya afya, makuzi, lishe, stadi za maisha na ubunifu. Sambamba na hayo Dkt. Sekela Mwakyusya ameongeza kuwa katika kambi hiyo wapo madaktari na wataalamu wasaikolojia ambao wanakaa na watoto hao katika kuwajenga kifikra na kuwapa elimu ya afya pamoja na lishe.

MATUKIO KATIKA PICHA:

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Lenard Subi mwenye miwani kulia akiwasili katika viwanja vya shule ya Nyakahoja akipokelewa na watoto walio katika kambi hiyo.

 

Watoto walio katika kambi ya nyakahoja chini ya shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI wakiimba nyimbo maalumu ya kuhamasisha kusonga mbele katika masuala ya afya.

 

Meneja Mawasiliano wa Shirika la AGPAHI, Jane Shuma akitoa ufafanuzi wa ratiba na mambo watakayofanya watoto katika kambi hiyo

 

Watoto, waandishi wa habari na baadhi ya wageni wakisikiliza kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza DKT Lenard Subi hayupo pichani.

 

Mtoto anayewakilisha Mkoa wa Mara akimuonyesha mgeni rasmi picha ya mti aliyochora ukionyesha malengo yake katika maisha.

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Lenard  Subi akipita kuangalia mambo ambayo vijana wabunifu wameyafanya kupitia kipengele cha mkali wao

ARTICLE CREDIT: http://www.kijukuu.com

More on News

Get Connected