SHIRIKA LA AGPAHI LAFUNGA KAMBI YA WATOTO ILIYOWEKWA JIJINI MWANZA,LAWATAKA WATOTO KUFUATA KANUNI ZA AFYA.

MENEJA WA KANDA WA SHIRIKA LA AGPAHI DR NKINGWA MABELELE AKITOA HOTUBA KATIKA SHEREHE ZA KUFUNGA KAMBI YA WATOTO JIJINI MWANZA.

MWANZA

SHIRIKA lisilo la kiserikali la AGPAHI limewasihi watoto kuzingatia Masomo, kanuni za afya kama zinavyoelekezwa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja kuwahamasisha watoto wengine kujiunga katika vikundi vya watoto.

Hayo yamesemwa leo na Meneja wa kanda wa Shirika hilo Dr Nkingwa Mabelele wakati wa kufunga kambi ya watoto iliyoandaliwa na shirika hilo iliyojumuisha watoto kutoka mkoa wa Mara, Simiyu na Tanga wenye umri kati ya miaka 9 mpaka 17.

Dr Mabelele amesema kuwa elimu ni msingi kwa kila mtoto hivyo watoto wanatakiwa kusoma kwa bidii na kuzingatia yale wanayofundishwa ikiwa ni pamoja na kufuatilia kanuni za Afya wawapo shuleni na Nyumbani.

Katika hatua nyingine Dr Mabelele amesema kuwa Shirika la AGPAHI limeendelea kutoa huduma za kisaikolojia kwa kupitia vikundi vya watoto na kwamba vikundi hivyo vipo katika vituo vya kutolea huduma za Afya za CTC.

Awali katika Risala yao, watoto hao wamelishukuru Shirika la AGPAHI kwa kuwaandalia kambi hiyo kwani imewasaidia kujifunza mambo mengi ya afya, makuzi, lishe, usafi binafsi pamoja na kufahamiana.

Sambamba na hayo watoto hao wameiomba Serikali iwaunge mkono Shirika la AGPAHI ili huduma za kisaikolojia kwa watoto kwa kupitia vikundi ziendelezwe na kuwafikia watoto wengi nchini.

Kwa upande wake, msaikolojia aliyekuwa na watoto kambini kwa muda wa wiki moja amewataka wazazi kuwasikiliza watoto na siyo kuwapiga na kuwatukana kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha watoto wajisikie wanyonge na wasiothaminiwa. Shirika la AGPAHI lilianzishwa mwaka 2011, hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu shirika limeweza kuwafikia jumla ya watu 189,806 kupata huduma za VVU/Ukimwi ikiwemo kupata dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV) na kati ya hao watoto wakiwa 8,615 sawa na asilimia 5%.

MATUKIO KATIKA PICHA:

WATOTO WAKIWA NA MENEJA WA KANDA WAKIKATA KEKI KATIKA SHEREHE HIYO.

MENEJA WA KANDA WA SHIRIKA LA AGPAHI TANZANIA DR NKINGWA MABELELE AKIMLISHA KEKI MMOJA WA WATOTO KUTOKA MKOA WA TANGA.

WATOTO WAKIONYESHA MAVAZI YAO YA UBUNIFU WALIYOTENGENEZA KWA KUTUMIA MAGAZETI

BAADHI YA WATOTO WAKIWA NA WATUMISHI WA AFYA WALIOAMBATANA NAO KUTOKA MIKOANI WAKISIKILIZA KWA MAKINI HOTUBA YA MGENI RASMI HAYUPO PICHANI.

MENEJA WA KANDA WA SHIRIKA LA AGPAHI TANZANIA DR NKINGWA MABELELE AKIWAGAWIA ZAWADI YA MABEGI WATOTO WOTE WALIOKUWA KATIKA KAMBI HIYO.

UTOAJI WA ZAWADI UKIENDELEA KWA WATOTO WOTE 50 WALIOHUDHURIA KATIKA KAMBI HIYO KWA MUDA WA SIKU 5.

MENEJA MAWASILIANO NA URAGBISHI WA SHIRIKA LA AGPAHI TANZANIA JANE SHUMA AKITOA UFAFANUZI WA KUKABIDHI VYETI KWA WATUMISHI WA AFYA.

MENEJA WA KANDA WA SHIRIKA LA AGPAHI TANZANIA DR NKINGWA MABELELEAKITOA ZAWADI NA CHETI KWA MTUMISHI WA AFYA ALIYEAMBATANA NA WATOTO KUTOKA MARA.

ZOEZI LA UTOAJI WA VYETI LIKIENDELEA KATIKA SHEREHE ZA KUFUNGA KAMBI YA WATOTO ILIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA NYAKAHOJA JIJINI MWANZA.

DR. MAIMUNA AHMED – DAKTARI WA WATOTO KATIKA KIPINDI CHA KAMBI AKIWAASA WATOTO KILA WAKATI KUZINGATIA MAELEKEZO YA WAHUDUMU WA AFYA.

WATOTO KUTOKA SIMIYU,TANGA NA MARA WALIOHUDHULIA KATIKA KAMBI HIYO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUKABIDHIWA ZAWADI NA MENEJA WA KANDA WA SHIRIKA LA AGPAHI TANZANIA DR NKINGWA MABELEL.

WATOTO KUTOKA SIMIYU,TANGA NA MARA WALIOHUDHULIA KATIKA KAMBI HIYO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATUMISHI WA AFYA NA WANASAIKOLOJIA WALIOKUWA KATIKA KAMBI HIYO.

PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUFUNGA RASMI KWA KAMBI YA WATOTO LEO KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA NYAKAHOJA JIJINI MWANZA.

More on News

Get Connected