MKUTANO WA AGPAHI NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA WAFANYIKA MJINI DODOMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akizungumza wakati wa mkutano wa waganga wakuu wa mikoa ambako shirika la AGPAHI linafanya kazi nchini Tanzania

“Shirika hili lilianzishwa mwaka 2011,kuanzia kipindi hicho tulikuwa tunafanya kazi zetu katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu, lakini kuanzia Oktoba 2016 Mikoa ya Mara,Geita,Tanga na Mwanza iliongezeka (tukitekeleza miradi ya Ukimwi) na mkoa wa Manyara uliongezeka ambako tunatekeleza  mradi wa kifua kikuu”,alisema Dk. Mwakyusa. 
 
“Tumekuwa tukifanya kazi zetu kwa kushirikiana kwa ukaribu kabisa na serikali. Na wafadhili wetu wakuu ni Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU kwa hisani ya Watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People (ADPP - Mozambique)”, aliongeza Dk. Mwakyusa. 
 
Aidha alisema mbali na mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi pia shirika hilo linatekeleza mradi wa kifua kikuu migodini kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu kifua kikuu kwa wachimbaji, familia zao na jamii inayowazunguka ili waweze kuchukua hatua za haraka kujikinga na kupata tiba sahihi ya kifua kikuu. 
Mradi huu hivi sasa unatekelezwa katika machimbo ya Iyenze na Mwime halmashauri ya Mji wa Kahama, Kakola na Mwazimba halmashauri ya Msalala katika mkoa wa Shinyanga pamoja na Mererani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ”,aliongeza Dk. Mwakyusa.
 
Kwa upande wao Waganga Wakuu wa Mikoa hiyo saba walilishukuru shirika hilo kwa jitihada zake za kujali afya za watanzania na kuahidi kuendelea kushirikiana na AGPAHI ili wananchi waweze kunufaika kupitia shirika hilo. 
 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dk.Asha Mahita akizungumza katika mkutano huo
 
 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk. Asha Mahita aliuhakikishia uongozi wa shirika hilo kuwa watakuwa wasimamizi wazuri wa fedha zinazotolewa na AGPAHI ili kutekeleza miradi iliyoanzishwa kwa faida ya watanzania. 
 “Kwanza nilipongeze shirika hili kwa kuongeza mikoa lakini pia kuamua kutukutanisha hapa, kwa kweli huu ni utaratibu mzuri na naomba tuendelee kushirikiana, sisi tupo tayari kuhakikisha tunasimamia miradi iweze kutekelezeka”, aliongeza Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk. Rashid Mfaume. 
 
Shirika la AGPAHI linajishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi, kutoa huduma ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kutoa huduma ya uchunguzi na huduma za awali ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa huduma za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, pia shirika hutoa vifaa tiba, kukarabati miundombinu ya vituo vya afya, kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya kwa msaada wa watu wa marekani. 
 
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MKUTANO HUO 
 Meneja Mawasiliano kutoka AGPAHI, Jane Shuma akiwakaribisha waganga wakuu wa mikoa katika ukumbi wa Morena Hotel mjini Dodoma kwa ajili ya kushiriki mkutano ulioandaliwa na shirika hilo. 
 
 Waganga Wakuu wa Mikoa saba wakimsikiliza Dk. Mwakyusa
 
 Mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la AGPAHI, Dk. Safila Telatela akiwasisitiza waganga wakuu wa mikoa kushirikiana na AGPAHI katika kufanikisha miradi ya masuala ya afya.
 
Meneja ruzuku kutoka AGPAHI ,Umboke Mwakilima akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya fedha za miradi inayotekelezwa na shirika hilo
 
Waganga wakuu wa mikoa wakisoma taarifa za masuala ya VVU na Ukimwi zilizotolewa na shirika la AGPAHI. Katikati ni Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi. Kulia ni Kaimu Mganga mkuu mkoa wa Simiyu, Dk. Chacha Magige .Wa kwanza kushoto ni Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Dk. Asha Mahita. 
  
 
 Picha ya pamoja: Viongozi wa shirika la AGPAHI na waganga wakuu wa mikoa ambako shirika hilo linafanya kazi zake
 
Picha zote na Malunde blog 
 

More on News

Get Connected