BONANZA LA MICHEZO LILILOANDALIWA NA AGPAHI LAKUTANISHA VIJANA 230 KUTOKA KISHAPU NA MANISPAA YA SHINYANGA

 

Kuadhimisha siku ya vijana duniani Agosti 12,2017, Vijana 230 kutoka halmashauri za wilaya ya Kishapu na Manispaa ya Shinyanga wamekutana katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

Bonanza hilo limefadhiliwa na Mfuko wa Kusaidia watoto wa Uingereza (Children’s Investment Fund Foundation UK- (CIFF) limefanyika Jumamosi Agosti 12,2017 katika uwanja wa shule ya msingi Kolandoto kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga.

Miongoni mwa michezo iliyochezwa na vijana hao ni pamoja mpira wa miguu,kuvuta kamba,mbio za magunia,kukimbiza kuku ,kuimba mashairi,kucheza muziki na kuonesha fasheni za mavazi ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kombe na mabegi ya shule.

Mgeni rasmi Afisa Tabibu wa hospitali ya Kolandoto,Maryciana Bruno akiongea wakati  wakati wa bonanza.

Akizungumza katika bonanza hilo mgeni rasmi Afisa Tabibu wa hospitali ya Kolandoto,Maryciana Bruno alisema lengo la bonanza hilo kwa ajili ya vijana kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha vipaji na kujifunza.

“Bonanza hili limejumuisha vijana wenye umri wa kati ya miaka 14-19 wanaotoka katika klabu za vijana ambazo zimeundwa na zinasimamiwa na AGPAHI kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya, vijana hawa wanatoka kwenye vikundi 10 vilivyopo katika halmashauri za wilaya mbili za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu,Manispaa ya Shinyanga”,alieleza Bruno.

“Nalishukuru sana shirika la AGPAHI kuendelea kuwa karibu na vijana hawa wanaopata huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo”,aliongeza. Aidha aliwataka viongozi wa halmashauri za wilaya kuendelea kutoa ushirikiano kwa shirika hilo hususani katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wananchi katika huduma za afya hususani kwa watu wanaopata tiba na matunzo ili huduma zipatikane katika ubora na ziwe rafiki kwa wananchi.

Afisa Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon Haule akiongea na vijana na wazazi waliojuuika kwenye bonanza hilo. 

Afisa Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon Haule aliwashukuru wazazi na walezi wa watoto na vijana kuendelea kushirikiana na AGPAHI kwa ukaribu zaidi huku akiiomba serikali kuendelea kulipa ushirikiano shirika hilo ili kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi yanafanikiwa zaidi.

Afisa Muuguzi Msaidizi katika kituo cha afya Kambarage Glory Assey akiwa na vijana.

Kwa upande wake Mlezi wa Vijana rika ambaye pia ni Afisa Muuguzi Msaidizi katika kituo cha afya Kambarage Glory Assey alisema mafanikio ya AGPAHI yanatokana na uwepo wa huduma rafiki zinazotolewa kwa watoto na vijana.

 Vijana walioshiriki bonanza wakiimba nyimbo ya kulishukuru shirika la AGPAHI kwa kuwathamini,kuwajali watoto na kuwapatia huduma muhimu.

 

 PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI

Afisa Tabibu wa hospitali ya Kolandoto,Maryciana Bruno akizungumza wakati wa kufungua bonanza hilo

Mlezi wa Vijana rika ambaye pia ni Afisa Muuguzi Msaidizi katika kituo cha afya Kambarage Glory Assey akitoa maelekezo kwa vijana namna ya kucheza mchezo wa kukimbia na mayai yaliyowekwa kwenye vijiko.

Wachezaji wa timu ya mpira ya kituo cha afya Kambarage wakijiandaa na mchezo.

Wachezaji wa timu ya mpira ya hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakijiandaa na mchezo dhidi yao na timu ya kituo cha afya Kambarage

Mchezo kati ya timu ya hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kituo cha afya Kambarage ukiendelea

Vijana wa Kambarage wakifurahia kombe lao la ushindi.

Mshindi wa mbio za mita 100 kwa upande wa vijana wa kike akifurahia wakati wa kumaliza mbio hizo.

Mshindi wa mchezo wa kukimbiza kuku akiwa ameshikilia kuku wake wa ushindi

Mshindi wa mbio za mita 100 upande wa vijana wa kiume akipokea zawadi ya begi

 

Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

More on News

Get Connected