WATU WAPATAO 1282 WAMEJITOKEZA KUPIMA NA KUTAMBUA AFYA ZAO MKOANI GEITA.

Shirika la AGPAHI kwa msaada wa watu wa Marekani kwa Kushirikiana na Halmashauri ya wilaya za Chato na Bukombe Mkoani Geita limeendesha zoezi la upimaji wa Virusi Vya UKIMWI(VVU) kwa hiyari na uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake wenye umri kuanzia miaka 30 na kuendelea.

Zoezi hilo la upimaji lilifanyika wilayani Chato katika Hospitali ya wilaya ya Chato, Kituo cha afya cha Bwanga, Zahanati ya buseresere na Nyabugera na Wilayani Bukombe katika Hospitali ya wilaya ya Bukombe, kituo cha afya cha uyovu na zahanati ya Bukombe.

Wanajamii wa Chato wakisikiliza kwa makini maelezo kwa afisa muuguzi  kuhusu shughuli ya upimaji katika hospitali ya wilaya ya chato

Kwa mujibu wa mratibu huduma unganishi kwa jamii mkoa wa Geita AGPAHI- Richard Kambaragwe amesema Jumla ya watu 1,282 wamejitokeza kupima HIV na UKIMWI na kati ya hao wa kike na wa kiume 36 wamebainika kuwa na maambukizi huku, wanawake wapatao 532 waliojitokeza kupima saratani ya mlango wa kizazi na wapatao 30 wamebainika kuwa na tatizo hilo.

Kambaragwe amesema Shirika hilo linaendesha huduma za upimaji kwa wananchi bila malipo hivyo Jamii imetakiwa kujenga utamaduni wa kupima Afya zao ili kujitambua mapema endapo kama watakuwa na maambukizi ya VVU na UKIMWI ama dalili za awali za saratani ya Mlango wa shingo ya Kizazi ambalo ni tatizo kubwa linalopelekea vifo vya watu wengi nchini na Duniani Kote.

Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative(AGPAHI) ni shirika la Kitanzania lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na Programu za kutokomeza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ,VVU na kuzuia maambukizi mapya ya VVU kwa watoto, kutoa tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania kwa kushirikiana na Serikali za Mikoa ,Serikali za mitaa na wahisani kwa msaada wa watu wa Marekani. Alisema AGPAHI imejikita katika kutoa msaada wa huduma zenye ubora wa hali ya juu na kuhakikisha jitihada za kufikia lengo la pamoja la kutokomeza maambukizi ya VVU kwa watoto linafikiwa ambapo huduma hizi hutolewa kwa msaada wa watu wa marekani.

Na huko Bukombe, Mratibu wa CTC wilaya Dr Romaria Malihera amewatahadharisha wananchi wasipuuze kwenda kupima afya na SARATANI ya Shingo ya kizazi kwani ugonjwa huo unaua kwa kutokujitambua mapema na ukishajitambua mapema kwa hatua ya awali unawezakupona lakini ukichelewa halina dawa .Watoa huduma kutoka wilaya za Bukombe na Chato na wale waliojitokeza kupima Afya zao kwa hiyari wameipongeza AGPAHI kwa msaada walioutoa wa kutoa huduma ya Upimaji UKIMWI na SARATANI ya Mlango wa shingo ya Kizazi Bure .

 

 

Wanajamii wakieendelea kupata huduma wakati wa zoezi la upimaji wa VVU

Aidha Revina Fadres na Mary Basinga kutoka wilayani Chato na wamewashauri wananchi wenzao kujitokeza kupima kila wanaposikia matangazo kwani kwa kuchukua hatua ya kupima unaweza kujitambua na hapo ndipo utaweza kuchukua hatua mapema kujilinda ama kujikinga au kuanza kutumia dawa.

Mashauri Charles na Rejina Sabini wakazi wa wilayani Bukombe waliwataka wanajamiii wenzao kuchukua hatua za haraka pindi watakapobainika kuwa na maambukizi ya aina ya VVU na kufuata ushauri nasaha kwa kutumia dawa ipasavyo kwani ukipuuzia maisha yako yatakuwa hatarini kuliko awali, walisisitiza kusema matumizi ya dawa sahihi hurefusha maisha yako ya kuishi.

Mashauri Charles, aliwatahadharisha wanaoanza kutumia dawa kuwa "wakijisikia nafuu huwa wanaanza kukimbia na kuacha kutumia dawa, hali hiyo ni hatari kwa afya kwani kifo kinaweza kukupata wakati wowote na kwa mateso makali hivyo akashauri jamii wasikataze kutumia dawa. Mashauri pia aliwashauri wanajamii  wawapuuze viongozi wa dini wale wanao wadanganya kwa maombezi kuwa wamepona hata kama imani zao zimepokea mapokeo wasiache kutumia dawa.

 

Wanawake kutoka wilaya ya Bukombe wakiketi kusubiri kupata huduma ya uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi

Huduma ya upimaji wa VVU ukiendelea katika wilaya ya Bukombe.

Zoezi hilo la upimaji lilifanyika wilayani Chato katika Hospitali ya wilaya ya Chato, Kituo cha afya cha Bwanga, Zahanati ya Buseresere na Nyabugera. Wilayani Bukombe katika Hospitali ya wilaya ya Bukombe, kituo cha afya cha Uyovu na zahanati ya Bukombe.

VIDEO FUPI WAKATI ZOEZI LA UPIMAJI LIKIENDELEA

 

NA MAKUNGA PETER,

GEITA.

More on News

Get Connected