AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI MKOA WA MWANZA

Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative( AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limetoa warsha kwa Waviu Washauri kutoka mkoa wa Mwanza ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).

 

 Mwezeshaji, Gladness Olotu akitoa mada ukumbini.

Warsha hiyo ya siku tatu iliyoanza siku ya Jumanne Novemba 28,2017 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza imekutanisha WAVIU washauri kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela,Kwimba,Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana.

"Waviu washauri" ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa, kutoa ushauri nasaha kwa wenzao,kujitolea kufuatilia  na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha Waviu kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.

 

Mgeni rasmi, Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza, Bi. Esperance Makuza,aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza akifungua warsha ya siku tatu ya watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza Jumanne Novemba 28,2017

Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo,Mgeni rasmi ambaye ni Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza Bi Esperance Makuza,(aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza, alisema Waviu Washauri wanayo nafasi kubwa ya kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya tiba na matunzo.

“Nyinyi ni viungo muhimu sana katika kuwaunganisha wateja na vituo vya kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU,hivyo mafunzo haya yatawafanya mpate ujuzi na uzoefu mzuri katika kuwahudumia wateja”,alieleza.

 

Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akielezea historia ya shirika la AGPAHI na shughuli zinazofanywa na shirika hilo nchini Tanzania

Naye Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona alisema shirika hilo linafanya kazi zaidi kwenye vituo vya huduma na limekuwa likijuhusisha zaidi na watoto.

Alisema shirika hilo sasa linatekeleza majukumu yake katika mikoa sita nchini ambayo ni Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Geita,Tanga na Mara. Mafunzo hayo yameandaliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC).

 

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA SEMINA YA WAVIU WASHAURI MWANZA  

Mwezeshaji Bi. Sherida Madanka akitoa mada wakati wa warsha hiyo.

 Washiriki wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa semina hiyo.

Mshiriki wa warsha hiyo Herman Ngika kutoka wilaya ya Magu, akichangia hoja ukumbini

 

Washiriki wa warsha hiyo wakiigiza namna ya kutoa ushauri nasaha kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
 
Mratibu wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA),kanda ya Mwanza,Bi. Veronica Joseph akitoa mada kuhusu hali ya maambukizi ya VVU nchini Tanzania na haki za watu wanaoishi na VVU.

 Picha zoteh na Malunde 1 blog

More on News

Get Connected