Shirika la AGPAHI latoa semina ya matumizi ya fedha za wafadhili Mjini Kahama

 

Serikali imewaagiza watumishi  wa sekta ya Afya katika mkoa wa Shinyanga na Geita,kutumia  vizuri fedha za miradi ya ukimwi zinazotolewa na wafadhili ili ziweze kuwafikia walengwa na kuacha tabia ya kujinufaisha wenyewe kupitia fedha hizo.

 Wito huo umetolewa leo na mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr Rashid Mfaume kwa niaba ya makatibu tawala wa mkoa wa Shinyanga na Geita,wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya usimamizi wa fedha yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI.

 Dr Mfaume amesema kumekuwa na tabia ya badhi ya watumishi wa Afya kutumia fedha za miradi ya wafadhili kwa kujinufaisha wenyewe huku walengwa wakikosa huduma muhimu ambazo zimekusudiwa kuwafikia.

 Sambamba na hayo Dr Mfaume amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa wa Shinyanga na Geita kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya ukimwi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watumishi watakaotumia vibaya fedha hizo.

  Wakiongea kwa niaba ya wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Shinyanga na Geita,Mkurugenzi wa Mbogwe Elias Kaendabila na mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Ally Swedi wamelishikuru shirika la AGPAHI na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata huduma.

  Kwa upande wake afisa Ruzuku mwandamizi wa Shirika la AGPAHI Leticia Gilba amesema kuwa,Shirika la AGPAHI Limetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 36 kwa muda wa mwaka mmoja kwa mikoa sita ya Tanzania bara huku mkoa wa Shinyanga ukipata shilingi Bilioni 6.4 na Mkoa wa Geita Shilingi bilioni 4.2.

   Akiitaja mikoa iliyopata fedha hizo Gilba amesema ni pamoja na Geita,Shinyanga,Mwanza,Tanga,Mara pamoja na mkoa wa Simiyu na kuongeza kuwa matarajio yao ni kuona fedha hizo zitatumika kama zilivyolengwa katika mikoa yote.

MATUKIO KATIKA PICHA: WAJUMBE WA SEMINA HIYO KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOA WA SHINYANGA NA GEITA WAKIWA KATIKA CHUMBA CHA MIKUTANO WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MGENI RASMI HAYUPO PICHANI.

Wajumbe wa semina hiyo kutoka halmashauri za Mkoa wa Shinynga na Geita wakiwakatika chumba chamikutano wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi hayupo pichani 

Afisa ruzuku mwandamizi wa Shirika la AGPAHI Leticia Gilba akifafanua jambo katika semina hiyo leo.

Mjumbe kutoka Ushetu akiuliza swali katika semina hiyo.

Wawakilishi kutoka halmashauri za Shinyanga na Geita wakiendelea na semina mjini kahama.

Kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya mbogwe mkoani Geita ,Elius kayandabila na wajumbe wengine katika siku ya pili ya semina hiyo 

 Afisa mradi mwandamizi wa shirika la AGPAHI, Julius Sipemba akitoa neno la shukrani kwa wajumbe waliohudhuria katika kikao hicho.

Mjumbe kutoka halmashauri ya Mbogwe akiuliza swali katika semina hiyo.

Wajumbe wakichangamsha mwili baada ya kukaa kwa muda mrefu 
 
Dr. Japhet Simeo,Mganga Mkuuwa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa mwenyekiti wa semina hiyo akitoa shukrani baada ya kufunga semina siku ya pili

Wajumbe wakiwa katika semina iliyoandaliwa na shirika la AGPAHI iliyofanyika katika hoteli ya Sub-Marine Mjini, Kahama.

 PICHA ZOTE NA KIJUKUU BLOG

More on News

Get Connected