Warsha ya WAVIU washauri Mkoa wa Shinyanga yafungwa. Watembelea hospitali ya mkoa na kituo cha afya, Kambarage

Kaimu Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI mkoa wa Shinyanga Sherida Madanka akizungumza wakati wa kufunga warsha ya siku tatu kwa WAVIU Washauri kutoka halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga.

Jumla ya WAVIU Washauri 75 kutoka halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga wamepatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma na kuwarudisha kwenye huduma za tiba na matunzo.

Mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa serikali ya Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control and Preventation (CDC) yalianza Januari 29,2018 na kumalizika Januari 31,2018 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kufunga warsha hiyo na kugawa vyeti vya ushiriki, Kaimu Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Shinyanga Sherida Madanka, aliwataka WAVIU Washauri kujitambua na kutoa elimu kuhusu haki za WAVIU katika jamii. Aidha aliwaasa WAVIU Washauri kutunza siri za wateja wanaowahudumia na kuhakikisha wanakuwa viongozi wa kuigwa katika jamii. 

“Ninaamini mtakwenda kutumia elimu mliyopata kuiemilisha jamii, mnatakiwa muwe kioo cha jamii ili wananchi wapate pa kukimbilia, hakikisheni mnatunza siri za watu mnaowahudumia”,alisisitiza Madanka. 

Alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la AGPAHI kwa huduma linalozotoa katika kutekeleza miradi ya Ukimwi huku akibainisha kuwa shirika hilo limekuwa kimbilio la wengi na mdau mkubwa wa masuala ya afya kwa serikali ya Tanzania. 

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUFUNGA WARSHA YA WAVIU WASHAURI 

Sherida Madanka akilishukuru shirika la AGPAHI kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kupambana na VVU na Ukimwi.

 Madanka akiwasisitiza WAVIU Washauri kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa jamii.

WAVIU Washauri wakimsiliza Sherida Madanka.

Sherida Madanka akikabidhi MVIU Mshauri Sospeter Richard cheti cha ushiriki wa warsha hiyo. Kushoto ni Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Morgan Mwita.

 

 Sherida Madanka akishikana mkono na Agnes John wakati wa zoezi la kugawa vyeti kwa washiriki wa warsha hiyo.

Kulia ni Mariam Wilson akipokea cheti cha ushiriki.

Kulia ni Michael Kabupu akifurahia wakati wa kupokea cheti cha ushiriki.

 Washiriki wa warsha hiyo wakifurahia baada ya warsha kufungwa.

 Picha ya pamoja washiriki wa warsha hiyo.

 

PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI SIKU YA PILI YA WARSHA YA WAVIU WASHAURI 

Mtoa huduma za afya katika kituo cha tiba na matunzo cha hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Elizabeth Lubasha akitoa maelezo kwa WAVIU Washauri namna wanavyohudumia wateja. Alisema wamekuwa wakihudumia wateja takribani 150 kila siku. 

Muuguzi / Mkunga kitengo tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga Grace Kali akionesha dawa za kufubaza makali ya VVU.

Muuguzi Msaidizi kitengo tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Eveline Kayanda

Mtoa huduma ngazi ya Jamii/MVIU Mshauri kutoka mkoa wa Mara, Judith Bwire akionesha mpangilio mzuri wa mafaili ya wateja.

Eveline Kayanda akionesha kitabu cha kumbukumbu za wateja.

 

Kulia ni Muuguzi katika kituo cha tiba na matunzo cha kituo cha afya Kambarage, Sabina Samwel akielezea utaratibu wanaoutumia kutunza kumbukumbu za wateja wanaofika katika kituo hicho.

 

PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI SIKU YA TATU YA WARSHA YA WAVIU KABLA YA WARSHA HIYO KUFUNGWA

Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi halmashauri ya Mji Kahama, Elibariki Minja akielezea namna ya kuandaa mpango kazi kwa WAVIU Washauri.

WAVIU Washauri wakifanya kazi ya kundi kuandaa mpango kazi

Kazi ya vikundi ikiendelea.

Brown Christian kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu akiwasilisha kazi ya kundi lake.

 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

 

 

 

 

More on News

Get Connected