PICHA 30: AGPAHI WATOA MAFUNZO KWA WAVIU WASHAURI SIMIYU

 

Mratibu wa kudhibiti UKIMWI mkoa wa Simiyu Dr. Khamis KulembaAkifungua Warsha ya siku tatu kwa Waviu washauri (Watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi washauri) iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi. 

Baadhi ya Waviu Washauri (Watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi washauri) kutoka katika Wilaya tano za Mkoa wa Simiyu wakiendelea na mafunzo yanayotolewa na Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi. 

Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi limeendesha warsha ya siku tatu kwa Waviu Washauri (Watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi washauri) kutoka wilaya za Busega na Maswa Mkoa wa Simiyu.
Warsha hiyo ilishirikisha jumla ya Waviu washauri 24 kutoka katika wilaya za Busega,Maswa, ambapo lengo likiwa ni kuwaongezea ujuzi na mbinu za kuwashawishi watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi waliocha kutumia dawa kuendelea na matumizi ya dawa.
 
Akifungua Warsha hiyo Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Simiyu Dr. Khamis Kulemba aliwataka Waviu washauri hao kutumia nafasi hiyo ya mafunzo kuhakikisha wanawarejesha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi 456 ambao wameacha kutumia dawa kwa mkoa huo.
 
Kulemba alisema kuwa ili kuweza kufanikisha hilo Waviu washauri wanatakiwa kutumia lugha nzuri, kuwa na upendo, kutumia njia za ushawishi zaidi pamoja na kuonyesha unyeyekevu wakati wakiwarudisha wagonjwa waliocha dawa.
 
Mratibu huyo alisema kuwa lengo la serikali pamoja na mkoa wa Simiyu ni kuhakikisha wanapunguza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, kuhakikisha wote wanaoishi na VVU na Ukimwi wanatumia dawa, pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi kwa asilimia 100.
 
Kwa upande wake Mratibu wa huduma unganishi mkoa wa Simiyu kutoka shirika la AGPAHI Herieth Novati, alisema shirika hilolimeamua kutoa mafunzo hayo ili kumaliza watu wenye VVU na Ukimwi waliocha kutumia dawa.
 
Mratibu wa huduma unganishi mkoa wa Simiyu kutoka shirika la AGPAHI Herieth Novati akitoa maelezo wakati wa warsha
 
Aidha Novati aliongeza kuwa lengo jingine ni kuhamasisha watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi kuunda vikundi vya watoto, ikina mama pamoja na vijana vitakavyohamasisha utumiaji wa dawa kwa wakati wote.
 
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo (waviu washauri) walisema kuwa wanategemea kupata ujuzi zaidi wa kuhakikisha watu waliocha kutumia dawa katika maeneo yao kurudisha na kuendelea kutumia dawa.
 
Paul Pita na Nhandi Bulengela walisema kuwa mafunzo hayo yatakuwa muhimu sana kwao katika kuboresha kazi yao ya ushauri na ushawishi kwa watu walioacha kutumia dawa.
 
MATUKIO KATIKA PICHA
Mratibu wa huduma unganishi mkoa wa Simiyu kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi Herieth Novati akiwasilisha mada kwa Waviu washauri wakati wa mafunzo hayo jana.
 
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
 
Mratibu wa UKIMWI Wilaya ya Maswa Elzabert Mushi akitoa mada kwa washiriki wa Semina juu ya umuhimu wa kufuatiliwa watu wenye Virusi vya Ukimwi na Ukimwi pamoja na uundaji wa Vikundi vya akina mama, watoto kwa watu wenye VVU.
 
Dr. Khamis Kulemba Mratibu wa kudhibiti UKIMWI mkoa wa Simiyu, akifungua warsha ya siku tatu ya Waviu washauri.
 
Paul Ngata kutoka Wilayani Maswa ambaye ni Viu Mshauri akitoa matarajio yake mara baada ya kumalizika mafunzo hayo.
 
Nhandi Bulengela Viu Mshauri kutoka Wilaya Busega akiongea katika mafunzo hayo.
 
 PICHA NA DERICK MILTON-SIMIYU NEWS
 

More on News

Get Connected