Shirika la AGPAHI lakabidhi Kompyuta na vifaa tiba Jijini Mwanza

 

Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano kwa ajili ya matibabu ya akina mama wanaogundulika na dalili za awali za maambukizi ya kansa ya shingo ya kizazi (Cryotherapy Machine) katika halmashauri za Sengerema, Kwimba na Ilemela mkoani Mwanza.Huduma hii hutolewa katika vituo vya kutolea huduma ya afya 20 katika mkoa wa Mwanza

Pia shirika hilo limekabidhi kompyuta 18 kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kutunzia taarifa za matumizi ya dawa za kufubaza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ARV’s pamoja na magonjwa nyemelezi.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa hii leo kwenye mkutano wa wadau wanaosaidia mapambano ya Ukimwi mkoani Mwanza, uliofanyika Jijini Mwanza ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI Dr. Sekela Mwakyusa anafafanua zaidi kuhusiana na vifaa hivyo.

Akitoa shukurani kwa niaba ya halmashauri zinazonufaika na vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mwl.Emmanuel Kipole amelishukuru shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na serikali ya Marekani kupitia Centres for Disease Control and Preventation (CDC) kwa kutoa vifaa hivyo.

Awali akifungua mkutano huo wa siku mbili kuanzia leo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewahimiza washiriki kujadili sababu za maambukizi ya virusi vya Ukimwi kuongezeka mkoani Mwanza ili kutoka na maazimio yatakayosaidia kushusha kiwango cha maambukizi hayo yaliyofikia asilimia 7.2 kwa takwimu za mwaka 2016/17.

Mratibu wa shughuli za Ukimwi mkoani Mwanza Dr.Pius Masele anasema elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi inapaswa kuendelea kutolewa katika jamii na kuhimiza vijana kushirikishwa zaidi kwenye elimu hiyo ikiwemo matumizi sahihi ya kondom pamoja na tohara salama kwa wanaume.

 

MATUKIO KATIKA PICHA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akipokea mashine ya kwa ajili ya matibabu kwa akina mama wanaogundulika kuwa na dalili za awali za maambukizi ya kansa ya shingo ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi wa AGPAHI Dr.Sekela Mwakyusa. Mashine moja inagharimu zaidi ya shilingi Milioni Sita.

Mashine hizo zitasaidia kutoa tiba kwa akina mama wanaogundulika kuwa na maambukizi ya awali ya kansa ya shingo ya kizazi.

Pia shirika la AGPAHI limekabidhi kompyuta 18 kwa ajili ya kutunzia taarifa za matumizi ya dawa za kufubaza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ARV’s pamoja na magonjwa nyemelezi kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza.

 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza kwenye mkutano huo.

Dr.Eva Matiko kutoka CDC akiwasilisha salamu zake kwenye mkutano huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI Dr.Sekela Mwakyusa akiwasilisha mada kwenye mkutano huo

Mkutano wa wadau wanaosaidia mapambano ya Ukimwi mkoani Mwanza.

 

PICHA NA VIDEO NA BINAGI BLOG,bmghabari

 

 

 

 

 

 

 

 

 

More on News

Get Connected