AGPAHI YAENDESHA MKUTANO WA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA RAFIKI KWA VIJANA

 

Mratibu wa shughuli za afya za vijana kutoka Shirika la AGPAHI, Jane Kashumba, akizungumza kwenye mkutano wa kuimarisha utoaji huduma Rafiki kwa vijana, kuwa vijana ni kundi ambalo linapaswa kusaidiwa katika makuzi yake kuanzia ndani ya familia ,mashuleni na hata kwenye vituo vya kutolea huduma za kiafya ,kwa kupewa elimu ya afya ya uzazi na madhara ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa na umri mdogo

Shirika lisilo la Kiserikali (AGPAHI) linalofanya shughuli zake hapa nchini za kuzuia maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi(VVU), na kuhudumia watu ambao walishaathirika na ugonjwa huo wakiwamo na watoto wadogo, limeendesha mkutano wa kuimarisha utoa huduma rafiki kwa vijana, kundi ambalo limekuwa likikabiliwa na changamoto katika makuzi.

Mkutano huo umeendeshwa kwa kushirikisha watoa huduma ya afya, wazazi, walimu, na maofisa maendeleo ya jamii, ambao wote hao wanatoka katika halmashauri Tano za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu, Ushetu, Msalala, Kahama mji, pamoja na manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza leo April 3,2018 kwenye mkutano huo mratibu wa shughuli za afya ya vijana kutoka Shirika hilo HILO Jane Kashumba, amesema kundi la vijana kwa asilimia kubwa limekuwa likikabiliwa na changamoto katika makuzi, hivyo wakaona ni vyema kukutana na wadau hao kujadiliana na kupanga mikakati namna ya kulisaidia ili lipate kuwa salama. 

“Lengo la kufanya mkutano huu na wadau hawa wa huduma za afya, wazazi, walimu na maofisa maendelo ya jamii, ni kuona namna tukakavyo wasaidia vijana katika utoaji huduma rafiki kwao, kuanzia majumbani, mashuleni, sehemu za huduma ya afya, pamoja na serikalini namna ya kuwatoa kwenye dimbwi tegemezi.”Amesema Kashumba. 

Ameongeza kuwa mtarajio ya mkutano huo ni kuona vijana wanaondokana na matatizo ambayo yamekuwa yakiwakabili kwenye ukuaji wao hasa rika balehe, ikiwamo kubakwa, mimba na ndoa za utotoni, magonjwa ya zinaa, maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi (VVU), pamoja na kupewa elimu ya kujitegemea na kuwezeshwa. 

Pia amewataka wazazi, walimu, na wahuduma wa afya kuvunja ukimya kwa vijana na kuwapatia elimu ya afya ya uzazi mara kwa mara wakiwapo majumbani, shuleni, sehemu za huduma za afya, na kuwa eleza madhara ya kujihusisha kimapenzi wakiwa katika umri mdogo. 

Nao baadhi ya wadau hao wa afya waliohudhulia mkutano huo wamelipongeza Shirika hilo la Agpahi kwa kusaidia makundi ya vijana kupatiwa elimu hiyo ya afya ya uzazi kupitia mradi wao wa huduma rafiki kwa vijana, ambao utasaidia kuwakinga vijana kupatwa na matatizo mengi katika makuzi yao likiwamo gonjwa la Ukimwi. 

SOMA PIA HABARI PICHA HAPA CHINI

Wadau wa utaoaji huduma rafiki kwa vijana wakiwa kwenye vikundi wakijadili namna ya kutoa huduma hiyo, changamoto zake pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ili vijana wabaki kuwa salama katika makuzi yao na kufikia umri wa utu uzima

 

Kundi la walimu likiendelea na majadiliano namna ya kutoa huduma rafiki kwa vijana wakiwapo mashuleni, changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi.

 majadiliano yakiendelea namna ya kuimarisha utaoa huduma rafiki kwa vijana

Kundi la watoa huduma wakiendelea na majadiliano kwenye mkutano huo wa kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana

 Majadiliano yakiendelea.

 

 

Kundi la wazazi likiwa katika majadiliano namna ya kuimarisha utoaji huduma Rafiki kwa vijana wakiwapo majumbani, changamoto zake na kuzitafutia ufumbuzi.

Kikundi cha watoa huduma ya afya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye majadiliano namna ya kuimarisha utoaji huduma rafiki kwa vijana kwenye vituo vya afya ikiwamo na kuwapa elimu ya afya ya uzazi, ili kujikinga na magonjwa ya zinaa, ukiwamo na ugonjwa wa Ukimwi.

 

Mery Marco akiwasilisha mada ambayo wameijadili kwenye kikundi chao cha wazazi namna ya utoaji huduma rafiki kwa vijana wao pindi wakiwa majumbani, kuwa ni kuvunja ukimya na kuwaeleza elimu ya afya ya uzazi, na kuacha mapenzi katika umri mdogo yakiwamo na madhara yake.

Anna neema Ntangwa akiwakilisha kundi la walimu, kuwa wao wataendelea na utoaji elimu ya makuzi, afya ya uzazi na stadi za maisha, kuteuwa walimu walezi ambao watakuwa wakitoa huduma rafiki kwa vijana na kutatua changamoto ambazo zitakuwa zikiwakabili katika mkuzi ya shuleni.

 

PICHA ZOTE NA SHINYANGA NEWS BLOG

More on News

Get Connected