×

Warning

Error loading component: com_users, Component not found.

AGPAHI YAFANYA BONANZA LA MICHEZO KWA VIJANA MKOA WA MWANZA

Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI limefanya bonanza la michezo kwa vijana kutoka halmashauri za wilaya mkoa wa Mwanza.

Bonanza hilo lililofadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC) limefanyika Ijumaa Aprili 27,2018 katika viwanja vya Lesa Garden Hotel Jijini Mwanza na kukutanisha vijana takribani 100 wenye umri kati ya 10 – 22 wanaotoka katika klabu za vijana zilizopo katika vituo vya tiba na matunzo (CTC). 
 
Akizungumza wakati wa kufungua bonanza hilo, Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona alisema vijana hao wanatoka kwenye vikundi 15 vilivyopo kwenye wilaya saba za mkoa wa Mwanza isipokuwa Ukerewe tu.
 
“Vijana wametumia bonanza hili kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki,kuonyesha vipaji na kujifunza mambo kadhaa ikiwemo kushiirikiana na kuendelea kuwa wafuasi wazuri wa huduma za afya hivyo kuboresha afya zao”,alieleza Cecilia.
 
“Naishukuru serikali ya Marekani kupitia AGPAHI kwa kuendelea kuwa karibu na vijana wanaopata huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo kwenye halmashauri za wilaya ambazo zimekuwa zikifanya kazi bega kwa bega na shirika la AGPAHI katika kuboresha huduma za afya”,aliongeza.
 
Hata hivyo alisema shirika la AGPAHI mkoani Mwanza limeanzisha klabu 15 zenye wastani wa vijana wa umri balehe kwa lengo la kuwakutanisha vijana hao kila mwezi ili wajifunze kwa pamoja masuala mbalimbali.
 
“Wakiwa katika klabu hizi vijana wanajifunza masuala ya msukumo rika kwa vijana,kushirikiana katika kutatua changamoto zao na njia za kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi”,alisema Cecilia.
 
Hata hivyo alitoa wito kwa viongozi wa halmashauri kuendelea kushirikiana na AGPAHI katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wananchi kwenye huduma za afya hususani watu wanaopata tiba na matunzo ili huduma zipatikane katika ubora na ziwe rafiki kwa watu wote.

Nao washiriki wa bonanza hilo walilishukuru shirika la AGPAHI kwa kuendelea kuwa karibu  na watoto huku wakieleza kuwa kupitia michezo wanajifunza mambo mengi ikiwemo kujiamini,kushirikiana na namna ya kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika maisha yao.

Miongoni mwa michezo iliyofanyika katika bonanza hilo ni pamoja na mbio za mita 100, kuvuta kamba,kukimbia na mayai,kukimbia na malimao, kunywa soda kwa haraka zaidi,mbio za magunia,maigizo na vichekesho ambapo kila mshindi na washiriki wote walipatiwa zawadi. 
 
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
 
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akizungumza wakati wa bonanza la michezo kwa vijana kutoka halmashauri za wilaya mkoa wa Mwanza
Cecilia Yona akielezea kuhusu umuhimu wa bonanza la michezo kwa vijana. Kushoto ni kiongozi wa vijana Joan John kutoka hospitali ya rufaa Bugando, kulia ni kiongozi wa vijana kutoka hospitali ya rufaa Bugando, Pudensia Mbwiliza.
Vijana wakimsikiliza Cecilia Yona.
 
Cecilia Yona akizungumza na washiriki wa bonanza hilo.
 
Cecilia Yona akiwashukuru wazazi na walezi kwa kuwaruhusu vijana kushiriki katika bonanza.
Cecilia Yona akitambulisha viongozi wa vijana wanaotoka katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza. Wa kwanza kulia ni Queen Mpina,akifuatiwa na Pudensia Mbwiliza,wa pili kushoto ni Joan John
 Vijana kutoka halmashauri ya wilaya ya Sengerema wakionesha mchezo wa igizo
 
 Vijana wakifuatilia igizo.
Burudani ya  Vichekesho ikiendelea.
 Vijana wakicheza kwa kuzunguka. 
Vijana wakiendelea kucheza uwanjani.
 Michezo inaendelea.
 
 Kulia ni Cecilia Yona akitoa maelekezo kwa vijana wakati wa mbio za mita 100 kwa vijana wa kiume.
Vijana wa kike wakikimbia mbio za mita 100.
Mbio za magunia zikiendelea kwa vijana wa kiume.
Mbio za magunia zikishika kasi kwa vijana wa kike.
Mbio za kukimbia na malimao kwenye kijiko zikiendelea
 Vijana wakiendelea na mchezo wa kukimbia na mayai kwenye vijiko huku wameweka mdomoni
 Mchezo wa kuvuta kamba nao ulikuwepo...hapo ni vijana wa kiume wakijiandaa kushindana kuvuta kamba na vijana wa kike.
Vijana wakiendelea na mchezo wa kuvuta kamba.
 
Cecilia Yona akiwauliza vijana nini wamejifunza katika bonanza hilo.
 
Kiongozi wa vijana Felix Joseph kutoka hospitali ya rufaa Bugando akiwasihi vijana kujiamini katika maisha.
 Cecilia Yona akikabidhi zawadi ya saa kwa mshindi wa mbio za mita 100 kwa vijana wa kike.
 Mshindi wa mbio za magunia akipokea zawadi ya saa
 Zoezi la kukabidhi zawadi ya chupa za maji kwa washiriki wote wa bonanza la michezo likiendelea.
 
 
Picha ya pamoja washiriki wa bonanza la michezo.
 
 
PICHA ZOTE NA MALUNDE 1 BLOG
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

More on News

Get Connected