SHIRIKA LA AGPAHI LAHAMASISHA JAMII MKOANI MARA KUPIMA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.

Neema Nyasary ambaye ni Afisa Mradi upande wa Mama na Mtoto kutoka Shirika la AGPAHI akitoa Elimu kwa akina Mama Umhimu wa Kupima Saratani ya Mlango wa Kizazi pamoja na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambapo kitaifa Maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Mara.

Wanawake ambao tayari wameisha pima vipimo vyao wakiendelea kunywa Soda pamoja na kula Biskuti huku wakisubiri Majibu yao. 

Vinywaji vilivyoandaliwa na Shirika la AGPAHI kwa ajili ya Watu watakaokuja Kupima Saratani ya Mlango wa Kizazi pamoja na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi katika Viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Mara.

Huduma ya Vipimo mbalimbali ikiendelea katika Viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Mara kwa kuandaliwa na Shirika la AGPAHI.

Muuguzi akitoa Ushauri kwa Mteja baada ya Kupima Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Shirika la AGPAHI chini ya Ufadhili wa Center For Diseases Control and Preventation (CDC )limehamasisha jamii Mkoani Mara kijitokeza kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake katika kuadhimisha siku ya wauguzi duniani tarehe 12 mwezi mei 2018. 

Akiongea na waandishi wa habari, Neema Nyasory ambaye ni afisa mradi upande wa mama na mtoto kutokashirika hilo amesema mwitikio wa wananchi katika kujitokeza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake pamoja na upimaji wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwiumekuwa mkubwa. 

Neema amesema kuwa tangu wameanza kuhamasisha suala hilo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambapo kitaifa nchini Tanzania yamefanyika Mkoani Mara kwa muda wa siku mbili wamefikia watu 127 na zoezi hilo bado ni endelevu katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa. “Katika maadhimisho haya kuna watu wengine wanapatiwa huduma kwenye viwanja vya mpira na sisi kama Shirika la AGPAHI tuko maeneo ya Hospitali ya Mkoa,Musoma.Wananchi wanakuja hapa tunawapa huduma” alisema Neema. 

Ameongeza kuwa katika vipimo hivyo akina mama wamebainika kuwa na magonjwa mengine tofauti naugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ambapo kati ya watu 127 ambao wameshapimwa mtu mmoja ndo aliyeweza kuwa na viashiria na amepatiwa matibabu. 

Pia, huduma hizo ni endelevu huku akiwataka wanawake kijitokeza kwa wingi kwa lengo ka kupima ili kujitambua na kuweza kuokoa vifo vya akina mama kutokana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi pamoja na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Maria Masanja,mkazi wa Nyakato, mjini Musoma amesema kuwa huduma aliyopata iliyoandaliwa na Shirika la AGPAHI ni tofauti na huduma ambazo wamekuwa wakipata hapo Nyuma. 

“Leo tumepokelewa kwa furaha wauguzi wetu wanatumia kauli nzuri pia tukipimwa na kumalizia tunakuja kupumzika sehemu yenye kivuli tunakunywa soda pamoja na biskuti hii hatujawahi fanyiwa sisi kama wagonjwa kwahiyo tumeona ni tofauti” alisema Maria. 

Shaban Togori,mkazi wa Kigera alisema kuwa wanaume hawana mwamko mkubwa wa kupima Afya zao kama wanawake hivyo ameitaka jamii kuendelea kupima ili kujua afya zao na kama mtu amepata maambukiziaweze kutumia dawa.

Akifunga Maadhimisho hayo Mh. Stella Alex ambaye ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa niaba ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi na ajira vijana na watu wenye Ulemavu Jenister Mhagama, amesema kuwa wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao kabla ya kutumia dawa huku akisisitiza jamii kuendelea kuchangia damu kwa lengo la kunusuru wagonjwa ambao wamekuwa wakifa kwa kukosa huduma ya damu salama. 

Naye Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania Paul magesa, amesema kuwa changamoto ya wauguzi ambao hawana ajira kwa sasa ni wengi ambapo amesema kuwa kwa nchi ya Tanzania kwa sasa inajumla ya wauguzi 45,000 na wanatoa huduma zaidi ya asilimia 60 kwa umma wa watanzania ambapo wauguzi 6,000 hawana ajira wako mtaani na ifikapo Agosti mwaka huuwauguzi 4,000 watahitimu na kufikia elfu kumi ya wauguzi ambao hawana kazi, hivyo ameiomba serikali kutoa ajira kwa wauguzi hao kwa lengo la kuondoa changamoto ya upungufu wa watumishi katika idara ya Afya. Kilele cha Maadhimisho siku ya Wauguzi duniani ufanyika Mei 12 Kila mwaka ambapo mwaka huu kitaifa Maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Mara huku kauli mbiu ikisema “Wauguzi Sauti ya Kuongoza Afya ni haki ya Binadamu.” 

Sehemu iliyoandaliwa na Shirika la AGPAHI kwa ajili ya kutolea huduma ya vipimo mbalimbali pamoja na Ushauri.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi Ajira , Vijana na Watu Wenye Ulemavu Mh Stella Alex akifafanua jambo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Mara.

Wauguzi kutoka Mikoa Mbalimbali ya Tanzania

Maandamano.

Mabangio yenye jumbe mbalimbali yakipita mbele ya Mgeni rasmi.

Wananchi wakipatiwa huduma katika Vibanda tofauti tofauti

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi Ajira , Vijana na Watu Wenye Ulemavu Mh Stella Alex akikagua Vibanda katiia Maadhimisho hayo.

   Burudani.

Rais wa Chama Cha Wauguzi Tanzania TANNA Paul Magesa akieleza Changamoto zinazowakabili katika Sekta ya Afya.

Viongozi Mbalimbali

 

 

 

More on News

Get Connected