SHIRIKA LA AGPAHI LAFUNGA KAMBI YA WATOTO NA VIJANA YA ARIEL CAMP 2018 MJINI MOSHI

Jumatatu ya Tarehe 11 Juni 2018 Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)   lilianza kambi maalumu ya watoto na vijana wa Mikoa mitatu ya Tanzania ambayo ni Mara, Shinyanga na Simiyu kati ya Mikoa sita inayofanya kazi na shirika la AGPAHI. Leo ikiwa imetimia siku ya tano na ya mwisho tokea mafunzo hayo ya kambi ya watoto yaanze.

 

Mgeni rasmi akiingia ukumbini akiwa ameongozwa na watoto waliopo chini ya shirika la AGPAHI.

Muwakilishii wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Uforo Mariki alifunga mafunzo hayo ya watoto na vijana katika hafla fupi ya ufungaji wa kambi hiyo inayojulikana kama ARIEL CAMP 2018 huku ikiwa na kauli mbiu “KIJANA EPUKA TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU.”

Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii kutoka mkoa wa Mwanza ambaye ndie mratibu wa ARIEL CAMP 2018 Bi. Cecilia Yona aliweza kuzungumza kwa ufupi lengo la kambi hiyo ni kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto na vijana. Washiriki wakiwa kambini hupata mafunzo ya afya pamoja na kushiriki kwenye michezo mbalimbali. Aliweza kutoa shukrani za dhati kwa walezi walioambatana na watoto, madaktari bingwa wa watoto, mtaalamu wa saikolojia, muelimishaji rika na wafanyakazi wa Shirika la AGPAHI kwa ushirikiano wao walioonesha katika kipindi chote cha kambi.

 

Mbali na mafunzo ya darasani, Bi. Cecilia alizungumzia juu ya ziara waliyofanya kwa washiriki wa Kambi kutembelea  ofisi za uhamiaji za Holili zilizopo katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Marangu kwenye geti la kupandia mlima Kilimanjaro, pia waliweza kutembelea nyumbani kwa Mzee Mumiro anayeishi karibu na geti la kuingia katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro na kujifunza mila na tamaduni za wachaga.

Naye Msaidizi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Mariki, katika hotuba yake aliweza kutoa pongezi kwa shirika la AGPAHI kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha watoto na vijana hao wanafikia malengo yao huku akiwapongeza watoto na vijana kwa kuweza kujifunza na kuonesha kwa vitendo kile walichojifunza kwa siku zote walizokua kambini hapo.

“Naona mambo yamekwenda vizuri na inaonesha hayo mliyoyapata yameingia mpaka kwenye damu, napenda kuwaambia kwamba hao wanaoshuhulika na nyinyi wanafanya kazi ya Mungu, sababu sisi hapa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na tunayoyafanya ni ya Mungu, na katika dunia hii ukiona mambo yanafanyika usifikiri yamekuja tu ni kwamba Mungu anakuja kwetu anatupa mawazo na tunafanya kwa kuelekeza maana Mungu anasema tusaidie wanao hitaji, na wahitaji wakubali kupokea na kufanyia kazi, na kwa haya mliyo yapata nadhani mtayatilia mkazo na mkiyatilia mkazo hamtapata shida yoyote, sababu watoto na vijana huwa mara nyingi wanahitaji kuelekezwa. Nalipongeza sana Shirika la AGPAHI kwa kuifanya kazi ya Mungu vizuri” Alisema Dr. Mariki.

Dr. Mariki alimaliza ufungaji wa kambi hiyo kwa kuwapatia watoto na vijana zawadi ambazo ziliandaliwa na Stanbic Banki wakishirikiana na Shirika la AGPAHI pamoja na kuwapatia zawadi na vyeti wahudumu wote wa afya waliombatana na watoto kwa kufanikisha kambi hiyo.

 

Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii kutoka mkoa wa Mwanza ambaye ndie mratibu wa ARIEL CAMP 2018 Bi. Cecilia Yona, akitoa shukrani zake za dhati kwa washiriki na wale wote waliowezesha kufanikiwa kwa ARIEL CAMP 2018.

Mmoja ya wawakilishi kutoka shirika la AGPAHI akiongea katika hafla ya kufunga kambi ya vijana na watoto 2018.

Muwakilishi kutoka Stanbic Banki akiongea wakati wa hafla fupi ya kufunga kambi ya watoto na vijana iliyofanyika kwa muda wa siku tano.

Mgeni rasmi Dr. Uforo Mariki akiongea na watoto pamoja na vijana walioshiriki katika ARIEL CAMP 2018, wakati wa kufunga kambi iliyoandaliwa na Shirika la AGPAHI.

WAtoto wakisoma ushairi uliokua umejaa ujumbe mzito ambao ulimgusa kila aliyekua katika hafla fupi ya kufunga kambi ya watoto na vijana iliyoandaliwa na shirika la AGPAHI.

Watoto waliokua wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa kufunga ARIEL CAMP 2018.

Mgeni rasmi alifurahishwa na kuamka kwenda kucheza na kuwatunza watoto walikua wakicheza mziki kwa furaha wakati wa kufunga ARIEL CAMP 2018.

Mmoja ya mtoto akionesha kwa vitendo moja ya mafunzo waliyofundishwa kwa njia ya ngonjera,.

Mgeni rasmi akiwa na watoto, vijana na wafanyakazi wa AGPAHI wakikata keki katika siku ya kufunga kambi ya kumi ya ARIEL CAMP 2018

Watoto, vijana, walezi, fanyakazi wa AGPAHI wakiwa na mgeni rasmi.siku ya kufunga kambi ya watoto na vijana ya 2018.

 

 

 

More on News

Get Connected