RC MONGELLA AFUNGA KIKAO CHA WADAU WA AFYA MKOA WA MWANZA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella amefunga kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoani Mwanza kilichofanyika kwa muda wa siku mbili Novemba 5 na 6 ,2018 katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.

Kikao hicho kilichofadhiliwa na Asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDs Health Initiative (AGPAHI) yenye malengo ya kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia nchini Tanzania,kililenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu afya.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho,Mheshimiwa Mongella amezitaka halmashauri za wilaya kuhusisha wadau wa afya wanapotengeneza bajeti zao ili kuhakikisha miradi mbalimbali inatekelezwa vizuri.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wadau wa afya mkoani Mwanza kushirikiana na kuhakikisha wanaboresha huduma ya mama na mtoto mkoani humo.

Aidha ameishukuru asasi ya AGPAHI kwa kujitolea kufadhili kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza huku akibainisha kuwa asasi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

 

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

 

Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella akifunga kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoani Mwanza kilichofanyika kwa muda wa siku mbili Novemba 5 na 6 ,2018 katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.

 

Wadau wa afya wakiwa ukumbini

Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella akifunga kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoani Mwanza 

Wadau wa afya wakiwa ukumbini

 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

More on News

Get Connected