Radio Programs Questions & Answers From Listeners

Please select your question Theme

Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanatokea kwenye vipindi vitatu;

  1. Wakati wa ujauzito: Mama mwenye VVU asipotumia dawa za ARV maalumu kwa ajili ya mama wajawazito anaweza kumuambukiza mtoto aliye tumboni
  2. Wakati wa uchungu na kujifungua: mama mjamzito mwenye VVU asipotumia dawa za ARV maalumu kwa ajili ya mama wajawazito anaweza kumuambukiza mtoto kwa kupitia maji maji na damu wakati wa uchungu na kujifungua.
  3. Wakati wa kunyonyesha: mama mjamzito mwenye VVU asipotumia dawa za ARV maalumu kwa ajili mama anayenyonyesha na mtoto kupata dawa kwa kipindi cha wiki 6 baada tu ya kuzaliwa, anaweza kumuambukiza mtoto VVU.