NDIO, YANAWEZA KUZUILIKA KWA NJIA ZIFUATAZO;
- Mama mjamzito kupata elimu ya kupima VVU na ushauri nasaha, kujua hali yake maambukizi mapema pindi anapojua ni mjamzito (Kliniki), pia hata baada ya kujifungua.
- Mama mjamzito anapogundulika ana maambukizi ya VVU anatakiwa kuanza dawa za kupunguza kiwango cha VVU (Viral suppression)
- Njia salama za mama mjamzito kujifungua
- Dawa za kinga kwa mtoto baada ya kuzaliwa (Nevirapine)
- Elimu na ushauri kwa mama anaenyonyesha namna bora/sahihi ya kumnyonyesha mtoto wake
- Ufuatiliaji wa karibu wa mtoto aliezaliwa na mama mwenye maambukizi ya VVU, mfano ukuaji wa mtoto, Chanjo, kinga za magonjwa nyemelezi, kipimo cha mapema cha VVU kwa watoto wadogo akiwa na wiki 4 – 8 (Dried Blood Sample)