en EN sw SW

FAQ

THEME 2 : MAAMBUKIZI YA VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

Je maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanaweza kuzuilika?

NDIO, YANAWEZA KUZUILIKA KWA NJIA ZIFUATAZO; Mama mjamzito kupata elimu ya kupima VVU na ushauri nasaha, kujua hali yake maambukizi…

NDIO, YANAWEZA KUZUILIKA KWA NJIA ZIFUATAZO;

  • Mama mjamzito kupata elimu ya kupima VVU na ushauri nasaha, kujua hali yake maambukizi mapema pindi anapojua ni mjamzito (Kliniki), pia hata baada ya kujifungua.
  • Mama mjamzito anapogundulika ana maambukizi ya VVU anatakiwa kuanza dawa za kupunguza kiwango cha VVU (Viral suppression)
  • Njia salama za mama mjamzito kujifungua
  • Dawa za kinga kwa mtoto baada ya kuzaliwa (Nevirapine)
  • Elimu na ushauri kwa mama anaenyonyesha namna bora/sahihi ya kumnyonyesha mtoto wake
  • Ufuatiliaji wa karibu wa mtoto aliezaliwa na mama mwenye maambukizi ya VVU, mfano ukuaji wa mtoto, Chanjo, kinga za magonjwa nyemelezi, kipimo cha mapema cha VVU kwa watoto wadogo akiwa na wiki 4 – 8 (Dried Blood Sample)
Posted 2 years agoby admin

Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanatokeaje?

Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanatokea kwenye vipindi vitatu; Wakati wa ujauzito: Mama mwenye VVU asipotumia…

Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanatokea kwenye vipindi vitatu;

  • Wakati wa ujauzito: Mama mwenye VVU asipotumia dawa za ARV maalumu kwa ajili ya mama wajawazito anaweza kumuambukiza mtoto aliye tumboni
  • Wakati wa uchungu na kujifungua: mama mjamzito mwenye VVU asipotumia dawa za ARV maalumu kwa ajili ya mama wajawazito anaweza kumuambukiza mtoto kwa kupitia maji maji na damu wakati wa uchungu na kujifungua.
  • Wakati wa kunyonyesha:mama mjamzito mwenye VVU asipotumia dawa za ARV maalumu kwa ajili mama anayenyonyesha na mtoto kupata dawa kwa kipindi cha wiki 6 baada tu ya kuzaliwa, anaweza kumuambukiza mtoto VVU.
Posted 2 years agoby admin