en EN sw SW

FAQ

THEME 4 : KIFUA KIKUU NA UKIMWI

Dalili za kifua kikuu ni zipi?

Kikohozi kwa wiki mbili au zaidi Makohozi yaliochanganyikana na damu Kupungua uzito Kutokwa jasho hasa wakati wa usiku Homa
  1. Kikohozi kwa wiki mbili au zaidi
  2. Makohozi yaliochanganyikana na damu
  3. Kupungua uzito
  4. Kutokwa jasho hasa wakati wa usiku
  5. Homa
Posted 2 years agoby admin

Kuna uhusiano gani kati ya UKIMWI na Kifua Kikuu?

Kifua Kikuu na UKIMWI ni magonjwa mawili yenye uhusiano ambapo kila ugonjwa huongeza kasi ya ugonjwa mwingine. Mtu anaweza kuishi…

Kifua Kikuu na UKIMWI ni magonjwa mawili yenye uhusiano ambapo kila ugonjwa huongeza kasi ya ugonjwa mwingine.

Mtu anaweza kuishi navimelea vya Kifua Kikuu bila kuugua kifua kikuu kama kingayake ya mwili ni imara.

  • Mtu anayeishi na VVU kinga yake ya mwili inapopungua husababisha vimelea vya Kifua Kikuu kuanza kushambulia mwili na kusababisha ugonjwa wa Kifua Kikuu.
  • Mtu anayeishi na VVU ni rahisi kuambukizwa na kuugua Kifua Kikuu kwani kinga ya miili yao hupungua.
  • Kifua Kikuu huharakisha mtu anayeishi na VVU kuugua UKIMWI.
  • Kifua Kikuu ni ugonjwa nyemelezi unaoongoza kusababisha vifo kwa watu wanaoshi na VVU.
  • Mtu anayeishi na VVU ana uwezekano mkubwa wa kupata Kifua Kikuu sugu

KUMBUKA: Sio kila mgonjwa wa kifua kikuu ana VVU na si kila anayeishi na VVU ana Kifua Kikuu

Posted 2 years agoby admin

Kuna uhusiano gani kati ya UKIMWI na kifua Kikuu?

Kifua Kikuu na UKIMWI ni magonjwa mawili yenye uhusiano ambapo kila ugonjwa huongeza kasi ya ugonjwa mwingine. Mtu anaweza kuishi…

Kifua Kikuu na UKIMWI ni magonjwa mawili yenye uhusiano ambapo kila ugonjwa huongeza kasi ya ugonjwa mwingine.

Mtu anaweza kuishi navimelea vya Kifua Kikuu bila kuugua kifua kikuu kama kingayake ya mwili ni imara.

  • Mtu anayeishi na VVU king ayake ya mwili inapopungua husababisha vimelea vya Kifua Kikuu kuanza kushambulia mwili na kusababisha ugonjwa wa Kifua Kikuu.