en EN sw SW

FAQ

THEME 5 : SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

Je ni mambo gani yanaweza kuongeza hatari ya kupata saratani hii kwa wanawake?

Mambo ambayo yanayoongeza hatari za kupata Saratani ya mlango wa kizazi ni kama ifuatavyo; Kushiriki tendo ndoa katika umri mdogo…

Mambo ambayo yanayoongeza hatari za kupata Saratani ya mlango wa kizazi ni kama ifuatavyo;

  • Kushiriki tendo ndoa katika  umri mdogo au chini ya miaka 18
  • Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofauti
  • Utumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system)
  • Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama Ukimwi
  • Uzazi wa mara kwa mara

 

Posted 1 year agoby admin

Je nini maana ya saratani ya mlango wa kizazi?

Saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya saratani inayosababisha vifo kwa wanawake wengi Tanzania , Saratani ya shingo ya…

Saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya saratani inayosababisha vifo kwa wanawake wengi Tanzania , Saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya saratani inayoshambulia chembe chembe hai zilizopo kwenye mlango wa kizazi (cervix) saratani hii husababishwa na virusi vya aina papilloma vijulikanavyo  kama Human Papiloma Virus(HPV)nambavyo huambukizwa kwa njia ya  kujamiana (ngono).

 Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi duniani. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea. Kwa Tanzania, wastani wa wanawake 6,241 huugua saratani hii kila mwaka, ambapo 4,355 kati yao hufa, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani (W.H.O) ya mwaka 2010

Posted 1 year agoby admin